PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: Kukaa Juu Namba Moja Juu ya Yanga Kuna Raha yake Bwana”-Haji Manara
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
Leo Jumapili Januari 28, 2018 muda huu timu ya Simba inacheza mchezo wa ligi kuu dhidi ya Majimaji kwenye uwanja wa taifa, kuelekea mechi...
Leo Jumapili Januari 28, 2018 muda huu timu ya Simba inacheza mchezo wa ligi kuu dhidi ya Majimaji kwenye uwanja wa taifa, kuelekea mechi hiyo afisa habari wa Simba Haji Manara amsema kukaa juu ya msimamo wa ligi kuna raha yake lakini haitakuwa na maana endapo watapoteza au kutaka sare kwenye mchezo wa leo.

“Wachezaji wetu wameahidi kujituma kuhakikisha tunapata pointi tatu ili kuendelea kukaa juu kwa uhuru zaidi, pale juu pana raha yake najua kwa matokeo yoyote ya mechi yetu na Majimaji tunaendelea kukaa juu, lakini haitakuwa na maana kama unakaa juu huku umefungwa au umetoka draw raha ya kukaa juu uwe umeshinda tena ushindi mzuri.”

Manara amesema majimaji ni timu nzuri wanaiheshimu kwa historia yake kwenye soka la bongo pamoja na rekodi yao nzuri ilipokutana na timu zinazofanya vizuri msimu huu.

“Ni timu nzuri yenye wachezaji wazuri na rekodi zao ni nzuri kwa timu ambazo zinafanya vizuri msimu huu Yanga, Singida United, Azam na hata Prisons hakuna timu iliyowafunga Majimaji kwa hiyo sisi hatuendi pale tukiwa tunawadharau, tunajua tunahitaji pointi tatu.”

Kuhusu presha ya Azam na Yanga ambazo zipo nyuma yao, Manara amesema, timu hizo haziwashughulishi wanachoangalia ni timu wanayokutananayo.

“Hawa wa nyuma tusishughulike nao sana, sisi tushughulike na na yule tunayecheza nae, tukishinda mechi zetu zote hawa wanyuma vyovyote itakavyokuwa hawatushughulishi. Lazima tuangalie anayekuja kucheza na sisi tusimwangalie Azam Yanga, Singida United hao tayari wapo nyuma yetu kama tutaendelea kushinda mechi zetu hata wafanye nini hawawezi kutufikia.”

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top