Katika kutekeleza maelekezo ya uboreshaji na ukarabati wa vituo vya
afya nchini, Mkoa wa Arusha amefanikiwa kuboresha vitua vya afya viwili
kwa awamu ya kwanza.
Akitoa taarifa fupi ya maendeleo ya ujenzi wa vituo hivyo,Mganga mkuu
wa Mkoa Dr.Vivian Timothy Wonanji, amesema mpaka sasa kwa mkoa wa
Arusha zoezi hili linaendelea vizuri na kwa kasi kubwa.
Awamu ya kwanza, Mkoa ulipata kiasi cha bilioni 1.4 kwa ujenzi wa
vituo viwili vya afya,ambapo ni kituo cha afya cha Nduruma kilipata
kiasi cha shilingi milioni 500 kwaajili ya ujenzi na milioni 200
kwaajili ya ununuzi wa vifaa na kituo cha afya cha Kambi ya Simba
kimepata milioni 500 kwaajili ya ujenzi na milioni 200 za ununuzi wa
vifaa.
Amesema kituo cha fya cha Nduruma kilichopo katika halmashauri ya
Arusha kinaendelea na ujenzi wa majengo matano na mpaka sasa yapo katika
hatua ya ukamilishaji,majengo hayo yakiwemo wodi ya wazazi na jengo la
upasuaji.
Kituo cha pili ni Kambi ya Simba kilichopo katika Wilaya ya Monduli,
ambapo mpaka sasa ujenzi unaendelea wa majengo nane yakiwa kwenye hatua
ya upauwaji.
Aidha,amesema katika awamu ya pili ya ujenzi wa vituo vya afya, mkoa
wa Arusha umeshaanza maandalizi yake kwa uundaji wa kamati mbalimbali
zakusimamia shughuli nzima na kiasi cha shilingi bilioni 1.2
zimeshatolewa na benki ya dunia kwa ujenzi wa vituo vya afya 3.
Wilaya ambazo zimepata fedha hizo ni, Wilaya ya Ngorongoro katika
ujenzi wa kituo cha afya cha Sakala, Wilaya ya Monduli kituo cha afya
cha Mto wa Mbu na Wilaya ya Longido ujenzi wa kituo cha afya cha
Engarenaiobor,ambapo kila kituo kitapatiwa kiasi cha shilingi milioni
400.
Pia, serikali imetoa fedha za ukarabati wa vituo vya afya mkoani
Arusha, kikiwemo kituo cha afya cha Murieti,kimepata kiasi cha milioni
700.
Kituo vingine ni kituo cha afya cha Usa liver ambacho kimepata kiasi
cha shilingi milioni 700 kwaajili ya ukarabati wa chumba cha upasuaji
kwa wakinamama.
Kituo cha afya cha Ololiendeki wilayani Longido nacho kimepata kiasi cha milioni 700 kutoka serikalini.
Dokta Wonanji amesema, mpango huu wa ukarabati wa vituo vya afya kwa
mkoa wa Arusha, awamu ya kwanza vituo vya afya 2 vimeweza kunufaika, na
awamu ya pili utakamilishwa kwa ukarabati wa vituo vya afya 6 na
kupelekea mpango huu kukarabati vituo vya afya 8 kwa mkoa mzima wa
Arusha.
Mpango huu wa ukarabati wa vituo vya afya upo katika awamu
mbili,yakwanza ilianza rasmi Septemba,2017 na utakamilika
Januari,2018,ambapo awamu ya pili umeanza Januari 2,2018 na utakamilika
Aprili,2018.
Post a Comment