(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU - DODOMA)
Na. MWANDISHI WETU -
DODOMA
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera,
Uratibu, Bunge, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama
ameitaka Halmashauri ya Wilaya ya Bahi kuhakikisha inamaliza ujenzi wa soko la
Kigwe kwa kuhakikisha wanajenga vyoo na vibanda vidogo vitakavyo saidia soko
hilo lililojengwa na Programu ya Miundo Mbinu ya Masoko, Uongezaji Thamani na
Huduma za Kifedha Vijijini (MIVARF).
Ameyasema hayo alipofanya ziara yake Wilayani Bahi Novemba 21,
2017 kwa lengo la kujionea namna uboreshaji wa soko hilo ambalo tayari
limekamilika kwa asilimia 90 na kukabiliwa na changamoto za vibanda na vyoo vya
kudumu.
“Ninaiagiza Halmashauri hii kuhakikisha inaleta timu ya
wataalamu kupima viwanja na kuvigawa kwa wananchi pamoja na kumalizia ujenzi wa
Vyoo vya soko ili lianzae utekelezaji wake haraka na kuhakikisha umeme
unafungwa ndani ya soko hili”.
Kwa upande wake Mbunge wa Bahi Mhe. Omary Badwel alieleza ujenzi
wa soko ni jambo ja muhimu linalogusa wanakigwe wote kwani tangu enzi za
mkoloni kumekuwa na changamoto ya soko na kuwataka wananchi kulitunza na
kuhakikisha linakuwa msaada kwao wote.
“Soko hili toka utawala wa mkoloni kulikuwa na soko bovu hivyo
hatua ya kulikamilisha litavutia wengi na kukuza uchumi wa wana Kigwe
wote.”Alisisistiza Badwel
Kwa upande wake mkazi wa Kigwe Bi.Anastazia Mkatato alieleza
kuwa kujengwa kwa soko hilo litatatua changamoto iliyopo ya kukosa soko la
kudumu kwani yaliyopo ni madogo yanayomilikiwa na watu binafsi.
“Ninaishukuru Ofisi ya Waziri Mkuu kupitia Programu ya Miundo
Mbinu ya Masoko, Uongezaji Thamani na Huduma za Kifedha Vijijini iliyoamua
kutujengea soko hapa Kigwe na hii itatupa nafasi ya kuuza mazao na bidhaa kwa
wingi kupelekea kukuza uchumi wetu.”Alieleza Anastazia.
Naye Mratibu wa Mradi Taifa Bw.Walter Swai alieleza kuwa soko
hili ni muhimu kwa wana Kigwe na maeneo jirani , hivyo tutaendelea kuunga mkono
jitihada za kuhakikisha vifaa vinawekwa ikiwemo Meza za kuuzia mbidhaa sokoni.
“Tayari Ofisi yangu itachukua changamoto hii ya kukosekana
kwa meza za kuuzia na kuitatua ndani ya mwezi mmoja hivyo niwaahidi kutekeleza
haya.”Alisisitiza Bw.Swai
AWALI:
Ujenzi wa soko la Kigwe umegharimu jumla ya zaidi ya
shilingi milioni 68 ambapo Ofisi ya Waziri Mkuu kupitia Programu ya Miundo
Mbinu ya Masoko, Uongezaji Thamani na Huduma za Kifedha Vijijini (MIVARF)
ilitoa kiasi cha zaidi ya shilingi Milioni 50 pamoja na Mfuko wa jimbo
kuchangia jumla ya shilingi Milioni 15. Dhumuni la mradi ni kuwa na eneo
rasmi la kufanyia biashara na kuwezesha wajasiliamali wa Kigwe na kujikwamua kiuchumi
na kukuza maendeleao yao.
Post a Comment