PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: RPC Kagera Afafanua Bomu lilivyoua Wanafunzi
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
Kamanda wa jeshi la polisi Mkoani kagera Agustino Olomi amesema chanzo cha wanafunzi kupoteza maisha na kujeruhiwa kwa bomu ni kutokana n...
Kamanda wa jeshi la polisi Mkoani kagera Agustino Olomi amesema chanzo cha wanafunzi kupoteza maisha na kujeruhiwa kwa bomu ni kutokana na Mwanafunzi kuokota bomu hilo akidhani chuma chakavu ili aweze kwenda kuuza.

Katika taarifa aliyoitoa akizungumza na Wanahabari Kamanda Olomi amesema kwamba katika kijiji hicho kumekuwa na tabia ya kuuza vyuma chakavu ambapo mnunuzi huwa akiwapatia malipo ya madaftari.

Kwa upande wa Kamanda wa Kikosi cha kulinda mipaka cha Jeshi la Wananchi wa Tanzania JWTZ wilaya ya Ngara Meja TR Mutaguzwa amesema Bomu hilo lilikuwa na vipande 36 na lingelipukia ndani ya darasa lingeleta athari zaidi

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top