PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: Edward Lowassa Ashangaa uvumi wa Kuhamia CCM....Afunguka Haya
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
Waziri mkuu wa zamani, Edward Lowassa amesema hana mpango wa kurejea CCM kama ambavyo taarifa zimekuwa zikisambazwa kwenye mit...


Waziri mkuu wa zamani, Edward Lowassa amesema hana mpango wa kurejea CCM kama ambavyo taarifa zimekuwa zikisambazwa kwenye mitandao ya kijamii.

Lowassa alisema jana Jumanne  kuwa  amepata taarifa za uvumi unaosambazwa kuwa kuna watu amewatuma kuomba arudi CCM jambo ambalo ni uongo.

"Huu ni uongo wa kutunga, wamekuwa wakitunga vitu vingi juu yangu, mimi sina mpango wa kurejea CCM," alisema Lowassa,ambaye ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema  .

Alisema uongo mwingine ambao unasambazwa ni kuwa Serikali imezuia watu kumtembelea nyumbani kwake jambo ambalo anaamini ni maneno yanayotungwa.

"Watu wanazuiwa kuja nyumbani kwangu, eti Serikali imezuia hivyo wanakuwa wanaogopa huu ni uongo Serikali haiwezi kuzuia watu kutembeleana," alisema

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top