Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Mary
Mwanjelwa akisalimiana na wajumbe wa kamati ya siasa mara baada ya kuwasili kuwasalimu
katika Ofisi za Chama Cha Mapinduzi Mkoani Mbeya akiwa ziarani Mkoani humo,
Jana Novemba 20, 2017. Picha zote Na
Mathias Canal
Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Mary
Mwanjelwa ambaye pia ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa akizungumza na
viongozi mbalimbali wa CCM Mkoa wa Mbeya mara baada ya kuwasili kuwasalimu katika
Ofisi za Chama Cha Mapinduzi Mkoani Mbeya akiwa ziarani Mkoani humo, Jana
Novemba 20, 2017.
Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Mary
Mwanjelwa akisalimiana na Katibu wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Mbeya Ndg Wilson
Nkambaku mara baada ya kuwasili kuwasalimu katika Ofisi za Chama Cha Mapinduzi
Mkoani Mbeya akiwa ziarani Mkoani humo, Jana Novemba 20, 2017.
Na Mathias Canal, Mbeya
Chama Cha Mapinduzi Mkoani Mbeya
kimemshukuru na kumpongeza Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John
Pombe Magufuli kwa kumteua Mhe Mary Mwanjelwa kuwa Naibu Waziri wa Kilimo
kuhudumu katika nafasi hiyo katika serikali ya awamu ya tano.
Pongezi hizo pamoja na shukrani
zimetolewa na Katibu wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Mbeya Ndg Wilson
Nkambaku kwa niaba ya wajumbe wa kamati ya siasa wakati akitoa taarifa ya
chama hicho Ofisini kwake Mara baada ya Naibu Waziri kuzuru katika Ofisi hizo
akiwa ziarani Mkoani Mbeya.
Nkambaku alisema kuwa Rais Magufuli
amefanya uteuzi muhimu kwani Mhe Mwanjelwa ni mchapakazi na msaada mkubwa kwa
chama hicho hivyo uteuzi huo umeonyesha Imani kwa Chama Cha Mapinduzi na
Wananchi wa Mkoa mzima wa Mbeya.
Aidha alimsihi Kutenda haki na
kufanya kazi kwa bidii huku CCM ikiahidi kutoa ushirikiano mwema Kwa Naibu
Waziri wa Kilimo na Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) Mkoani Mbeya.
Akizungumza na viongozi wa Chama Cha
Mapinduzi na Jumuiya zake kwenye Ukumbi wa Ofisi za CCM Mkoa wa Mbeya Naibu
Waziri wa Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa aliwasihi makada hao Kutofanya kazi za
Chama kwa Mazoea badala yake kufanya kazi kwa weledi ili kuwasaidia wanachama
na wasiokuwa wanachama wa CCM katika shughuli za maendeleo.
Naibu Waziri Huyo ambaye ni Mjumbe
wa Halmashauri kuu ya Chama Cha Mapinduzi Taifa (MNEC) amejivunia malezi bora
na muhimu aliyoyapata ndani ya Chama Cha Mapinduzi huku akiwasihi viongozi
kuongeza bidii katika kumsaidia Rais Magufuli kutimiza ndoto ya Tanzania Mpya
kwa manufaa ya watanzania katika kuwaletea maendeleo.
Post a Comment