Kaimu Mkuu wa Kitengo cha
Mawasiliano (NIDA) Bi. Rose Joseph (mwenye miwani) akizungumza na baadhi
ya waandishi wa Vyombo vya Habari vya Televisheni na Magazeti
walipotembelea kituo cha usajili cha Sombetini, Arusha mjini kuangalia
shughuli za kuwasajili wananchi zinazoendelea kituoni hapo.
Wananchi wakiendelea kupata huduma
za usajili kabla ya kupigwa picha kama wanavyoonekana pichani. Wananchi
hao ambao ni kutoka Kata ya Sombetini wamekuwa wakijaziwa fomu na
kugongewa mihuri na wenyeviti kwenye mitaa wanayoishi kabla ya
kusajiliwa kwenye mfumo wa NIDA.
Hapa ni Mwenyekiti wa mojawapo ya
mitaa ya Kata ya Sombetini (mwenye kofia) akigonga mhuri kwenye fomu ya
mwananchi kuthibitisha kumtabua, na mkazi wa eneo lake.
Moja ya mashine aina ya BVR ikiendelea kuwasajiliwa wananchi wa Kata ya Sinoni waliopanga foleni kupata huduma ya Usajili.
Baadhi ya wakazi wa Kata ya Sinoni
Arusha wakiwa kwenye foleni ya kupigwa picha baada ya kukamilisha hatua
za awali za Usajili ambazo ni kujaza fomu za maombi na kuthibitishwa na
Idara ya Uhamiaji.
Akina mama pamoja na jukumu la
malezi wamejitokeza kusajiliwa kama anavyoonekana pichani mmoja wa
akinamama wa Kata ya Sinoni akiwa amembeba mtoto wake mkono mmoja na
mkono mwingine akiwa anaendelea na hatua za usajiliwa.
…………….
Baadhi ya waandishi wa Habari
kutoka vyombo mbalimbali vya Habari zikiwemo Televisheni na Magazeti
Jana walitembelea vituo vya Usajili mkoa wa Arusha kuona hatua za
usajili na mwitikio wa wananchi katika kupata haki yao msingi ya
kikatiba ya kusajiliwa.
Wananchi wa Mkoa wa Arusha
wameendelea kujitokeza kwa wingi kujisajili Vitambulisho vya Taifa; huku
idadi ya Kata za Usajili zikiongezeka. Moja ya Kata iliyoanza Usajili
jana kwa upande wa Wilaya ya Arusha mjini inaendelea kuwasajili wananchi
katika Kata ya Themi, Sekei, Sombetini na wameongeza Kata nyingine ya
Sinoni.
Wilaya ya Monduli inakamilisha
usajili kwenye Kata za Monduli Mjini, Monduli Juu na Engutoto;
ikijipanga kuendelea na Kata za Lashaine, Sepeko, Meserani na Mfereji.
Kwa Upande wa Arumeru Kata zinazofanya Usajili ni Musa, Ambureni,
Leburuki, Imbasenyi na Ngabobo, Longido ni Kata za Olubomba, Namanga na
Kimokoa na wanajiandaa na Kata za Kamwanga, Tingatinga, Olumorodi na
Sinya. Karatu wanaendelea na Usajili kwenye Kata ya Karatu na Rhotia
kabla ya kuhamia Ganako. Wilaya ya Ngorongoro wameanza na Tarafa ya
Ngorongoro kabla ya kuanza Mitijo.
Uongozi wa Mkoa umejizatiti
kuhakikisha wananchi wote wanasajiliwa kwa wakati na kupata Vitambulisho
vya Taifa vitakavyowawezesha kushiriki katika shughuli mbalimbali za
uzalishaji mali pamoja na upatikanaji kirahisi wa huduma za kijamii.
Post a Comment