Abate
wa Pambu Martin Mkolwe Abasia ya Mvimwa akiongoza ibada fupi ya
kuwaombea marehemu wa ajali iliyoua watu 15 na kujeruhi 9 iliyofanyika
katika kituo cha afya Mvimwa, Wilayani Nkasi.
Mkuu
wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen (kaunda Suti ya ugoro)
akitoa salamu zake za pole kwa wafiwa, kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya
Nkasi Mh. Said Mtanda na kuliani kwake ni Abate Pambu Mkolwe wa Abasia
ya Mvimwa.
………….
Uongozi
wa Mkoa wa Rukwa chini ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kmaishna Mstaafu Zelote
Stephen umeungana na ndugu wa majeruhi 9 na wafiwa wa vifo vya watu 15
vilivyotokea katika ajali ya lori aina ya fuso eneo la Ntembwa, Wilayani
Nkasi.
Katika
kuhakikihsa tukio hilo halijirudii Mh. Zelote amepiga marufuku
ukiukwaji wa sheria ya kupandisha abiria katika magari ya mizigo na
kuonya kuwa yeyote atajayefanya hivyo achukuliwe hatua haraka
iwezekanavyo.
“Nimekataza
binadamu kugeuzwa kuwa ni mifuko ya misumari, ni bora tubakie na
wananchi wetu salama, watu wasipande kwenye malori, nimefikiria ni vyema
tutumie zile chai maharage kuliko kupanda kwenye malori,” Alisisitiza.
Mh.
Zelote alifika katika eneo la tukio mara tu baada ya kupokea habari
hiyo ili kuweza kusaidia na kuhakikisha maiti na majeruhi hao wanapatiwa
huduma stahiki na kufanikisha zoezi la uokoaji.
Ajali
hiyo ilitokea baada ya lori aina ya fuso yenye namba za usajili T 425
BFF kuacha njia na kupinduka ilitokana na mwendo kasi wa dereva
uliochangiwa na ugeni wa barabara hiyo.
Lori
hiyo mali ya Bakari Ali Kessy iliyokuwa imetokea Kijiji cha Mvimwa
kuelekea Kijiji cha Wampembe ilikuwa imepakiwa shehena ya viroba vya
mahindi na watu iliacha njia, kupinduka na kusababisha vifo vya watu 15
kati yao wanawake 10 na wanaume 05.
Waliofariki katika ajali hiyo ni
- Domona Tenganamba, 41yrs, mfipa mkulima.
- Emmanuel Rashid 84yrs, mfipa mkulima, mkazi wa ntemba
- Restuta Sunga , 35yrs, mfipa mkazi wa ntemba
- Salula Revana 64yrs, mfipa mkazi wa mtapenda isale
- Ferisia Tenganamba , miaka 1 – 6/12
- Prisca Madeni, 45yrs, mfipa, mkulima, mkazi wa china
- Richard Chikwangara, 24yrs, mfipa, mwalimu mkazi wa kalambanzite
- Yusta Somambuto, 36yrs, mfipa, mkulima mkazi wa kizumbi
- Gilesi Ramadhan, 24yrs, mfipa, mkulima mkazi wa sumbawanga
- Odetha Madirisha 46yrs, mfipa mkulima wa kizumbi
- Megi Nalunguli, 52yrs, mfipa, mkulima mkazi wa wampembe
- Abuu Amani @ mandevu, 37yrs, muha, biashara, mkazi wa liapinda
- Nyandindi Batrahamu, 35yrs, mfipa, mkulima, mkazi wa sumbawanga
- Magdalena Mbalamwezi, 50yrs, mfipa, mkulima mkazi wa ntuchi
- Mtoto mchanga wa wiki mbili, mwanaume ambaye hajapewa jina
Majeruhi wa ajali hiyo ni:-
- Dismas Clement, 26yrs, mfipa, mkulima mkazi wa mwinza
- Sema Savery 25yrs, mfipa, mkulima mkazi wa wampembe
- Ally Haruna, 33yrs, mfipa, mkazi wa namanyere
- Yusta Mfundimwa, 50yrs, mkulima mkazi wa izinga
- Tenesfory Oscar, 36yrs, mfipa mkazi wa wampembe
- Amos Kitambale, 25yrs, mfipa, mkazi wa wampembe
- Neema Mwanandenje, 21yrs, mfipa, mkazi wa mlambo
- Joseph Sungula, 28yrs, mfipa, mkulima.
- Majeruhi mmoja mwanamke ambaye hajafahamika kwa jina yuko icu
Baada ya kusababisha ajali hiyo dereva alitoroka lakini juduhudi za kumtafuta mtuhumiwa zinaendelea kufanyika.
Post a Comment