PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: TASWA DAR YAKOMBA ZAWADI ZOTE TAMASHA LA 13 LA WANAHABARI ARUSHA MBELE YA RC GAMBO
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo akitoa nasaha kwa wachezaji wa mpira wa pete TASWA QUEENS DSM na TASWA ARUSHA QUEENS katika mchezo uli...
Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo akitoa nasaha kwa wachezaji wa mpira wa pete TASWA QUEENS DSM na TASWA ARUSHA QUEENS katika mchezo ulioisha kwa Taswa queens DSM kujinyakulia ushindi mnono

Katibu wa Taswa Arusha Mussa Juma akizungumza na wanahabari juu ya historia ya tamasha la 13 la wanahabari mkoani Arusha  na kutoa fursa kwa  mwenyekiti wa Taswa Arusha Jamila Omari kuzmkaribisha mgeni rasmi wa tamasha hilo mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo.

Mwenyekiti wa Taswa FC Majuto Omari akizungumza na wanahabari waliojitokeza katika tamasha la wanahabari mkoani Arusha lililofanyika katika viwanja vya general tyre.

Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo akikagua timu ya taswa queens  kutoka Daresalaam kabla ya mchezo wa kuvutia kati yao na Taswa Arusha na kujinyakulia ushindi wa magoli 19 dhidi ya 7 ya TAswa Arusha ambapo walipewa kombe na fedha taslimu kiasi cha shilingi laki moja.

Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho gambo akikagua timu ya Sunrise radio kabla ya mchezo wao na radio Five katika tamasha la wanahabari mkoani Arusha

Katibu wa Taswa Arusha Mussa Juma akizungumza na wanahabari juu ya historia ya tamasha la 13 la wanahabari mkoani Arusha  na kutoa fursa kwa  mwenyekiti wa Taswa Arusha Jamila Omari kuzmkaribisha mgeni rasmi wa tamasha hilo mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo.

 
Timu ya mpira wa miguu ya waandishi wa habari za michezo nchini (Taswa FC) na ya mpira wa pete (Taswa Queens) zimetwaa ubingwa wa tamasha la 13 la vyombo vya habari la Arusha (Arusha Media Bonaza) lililofanyika kwenye viwanja vya General Tyre.
Wakati Taswa FC ikitwaa nafasi ya kwanza kwa mpira wa miguu baada ya kujikusanyia pointi saba, Taswa Queens ilitwaa nafasi ya kwanza kwa upande wa netiboli baada ya kuifunga Taswa Arusha kwa mabao 19-7 katika mchezo wa kusisimua ulioshuhudiwa na Mkuu wa Mkoa wa  Arusha, Mrisho Gambo.

Akizungumza katika ufunguzi wa tamasha hilo mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo amesema kuwa michezo ni afya na ajira kwa vijana wengi kwa sasa na wanahabari kama tasnia inayounganisha jamii kubwa haina budi kuendeleza michezo mbalimbali  ili kuhakikisha jamii inapata uelewa wa kutosha juu kukuza na kuendeleza vipaji vyao.
Aliipongeza taswa fc na taswa queens kwa kuleta changamoto katika tamasha hilo na kiziasa timu za vyombo vya habari Arusha kujenga utamaduni wa kuwa na michezo ya mara kwa mara ili kujiweka fiti muda wote vinginevyo watakuwa wakifungwa kila tamasha la wanahabari linapofanyika na kuwaachia taswa fc na taswa queens kutoka Daresalaam kujinyakulia ushindi huo mara kwa mara.
Aidha ametoa changamoto kwa kamati ya maaandalizi ya bonanza hilo kuangalia namna ya kuliboresha bonanza hili kwa kuongeza timu nyingine kama za serikali ya mkoa, watu wa bodaboda na tasnia nyingine ili kuleta mshikamano jijini Arusha. 
 Mwenyekiti wa Taswa Arusha Jamila Omari amemshukuru mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo kwa kuukubali mwaliko wa kuwa mgeni rasmi katika tamasha hilo na nasaha alizotoa kwa wanahabari mkoani Arusha kuwa wazingatie kufanya mazoezi ya mara kwa mara uli wawe na afya bora na wasisubiri mpaka bonanza ndiyo wacheze mpira.

Katibu Mkuu wa Taswa Arusha, Mussa Juma alizipongeza timu zote kwa kushiriki katika bonanza hilo ambalo lilidhaminiwa na  Hifadhi za Taifa (TANAPA) Mifuko ya hifadhi ya Jamii ya LAPF na PSPF, Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro, kampuni ya bonite botllers LTD kupitia kinywaji chake cha  Coca Cola, Tanzania breweries LTD, kampuni ya ya vinywaji baridi ya SBC (T) Limited kupitia kinywaji chake cha Evervess na Arusha Palace Hotel ambapo alitaja timu zilizoshiriki katika tamsha hilo kuwa ni waandaji wenyeji wa tamasha hilo Taswa Arusha, Sunrise radio, Radio five Arusha na wageni pekee timu ya Taswa fc kutoka Daresalaam
Mbali ya Taswa FC kutoka Daresalaam  kutwaa vikombe vya mpira wa miguu, timu hizo ambazo zinadhaminiwa na kampuni ya MultiChoice Tanzania (DSTV), benki ya TPB na Property International Limited, pia ilihakikisha vyombo vya ha ari vya Arusha vinaondoka  mikono mitupu baada ya kutwaa nafasi ya kwanza katika mbio za kufukuza kuku. Magret Elia ambaye ashinda kuku wawili na Veronica Deus aliyeshinda mara moja.
Taswa FC ilianza kampeni yake kutetea ubingwa wake kwa kutoka sare ya 1-1 dhidi ya Radio Sun Rise. Timu hiyo ilisawazisha kupitia kwa Zahoro Mlanzi  baada ya gonga safi za  Wilbert Molandi, Ali Salum na Saidi Seif.
Taswa FC ilibadili upepo wa mashindano hayo baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Taswa Arusha baada ya Ibrahim “Maestro” Masoud kufunga kwa penati na Nicholas Ndifwa kufunga la pili baada ya ushirikiano mzuri wa Martin Shilla, Edward Mbaga, Kulwa Ndege na Muhidin Sufiani.
Mchezo wa kuamua nani bingwa ulikuwa kati ya Taswa SC dhidi ya Radio 5 ambapo Saidi Seif alifunga bao la ushindi kufuatia pasi ya Mohamed Akida aliyecheza vizuri na Majuto Omary.
Timu ya netiboli, Taswa Queens ilishinda mchezo wa fainali kwa mabao 19-7, mchezo ambao ulihudhuliwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo.
Taswa Arusha iliongoza dakika za mwanzoni mwa mchezo kabla ya Taswa Queens kubadili kibao na kuongoza kwa 10-5 mpaka mapumziko. Sharifa Mustafa, Veronica Deus na  Imani Makongoro walifunga kwa  Taswa Queens ambapo Zuhura Abduknoor, Magreth, Elia, Elizabeth Mbassa,  Amina Abdallah, Rukia Juma, Dosca Munthali alihakikisha Taswa Arusha ambayo ilikuwa chini ya  Rehema Mussa haifurukuti.
Kwa matokeo hayo, Taswa  SC zilitwaa kombe na fedha taslimu Sh 300,000. Mwenyekiti wa timu hiyo, Majuto Omary aliwapongeza wachezaji wake na wadhamini, Benki ya TPB, DSTV na Property International Limited kwa kufanikisha safari hiyo.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top