Naibu Waziri wa Fedha na Mipango
Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (kushoto) akizungumza na Afisa Mtendaji
Mkuu wa Kiwanda cha Sukari cha Kagera Bw. Ashwin Rana alipotembelea
kiwanda hicho kwa ziara ya kikazi ambapo alimpongeza kwa kuongeza
uzalishaji wa Sukari na kutoa ajira kwa wakulima wanaozunguka eneo hilo.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango
Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (kulia) akiongozwa na Afisa Mtendaji Mkuu
wa Kiwanda cha Sukari cha Kagera Bw. Ashwin Rana alipotembelea kiwanda
hicho kwa ziara ya kikazi.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango
Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (wa pili kushoto) akipata maelezo kutoka
kwa Mhandisi wa masuala ya Kielektroniki wa Kiwanda cha Sukari cha
Kagera, Bw. Obed Kiswaga (kushoto) kuhusu utendaji kazi wa kiwanda hicho
baada ya kutembelewa na Naibu Waziri huyo.
Msimamizi wa Mitambo ya Kiwanda
cha Sukari cha Kagera, Bw. Eliasa Kilemile (kushoto) akitoa ufafanuzi
wa usimamizi wa mitambo ya kiwanda hicho kwa Naibu Waziri wa Fedha na
Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (kulia) baada ya Naibu Waziri huyo
kufanya zaiara kiwandani hapo.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango
Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) akiwa ameshika mfuko wa sukari wenye ujazo
wa kilo moja inayozalishwa katika Kiwanda cha Sukari cha Kagera,
alipokuwa akipata maelezo kuhusu ubora wa sukari inayozalishwa kiwandani
hapo kwa kutumia teknolojia ya kisasa.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango
Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (kushoto) akiangalia mitambo ya kutengeneza
Sukari inavyofanyakazi, alipotembelea katika kiwanda cha Sukari cha
Kagera.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango
Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (wa pili kushoto) akitembelea maeneo ya
kiwanda cha Sukari cha Kagera kujionea namna kiwanda hicho
kinavyozalisha sukari.
Mtaalam Mwandamizi wa masuala ya
Kilimo katika kiwanda cha Sukari cha Kagera, Bw. Nassoro Abubakari, (wa
pili kulia) akimuelezea Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe Dkt.
Ashatu Kijaji (Mb) (kushoto) kuhusu mbegu tano za miwa ambazo zinatumika
katika shamba la miwa la kiwanda hicho.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango,
Mhe Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (kushoto) akisikiliza maelezo ya Mtaalam
Mwandamizi wa masuala ya Kilimo katika kiwanda cha Sukari cha Kagera,
Bw. Nassoro Abubakari, kuhusu ramani ya shamba la kiwanda hicho na namna
linavyotumika katika uzalishaji wa miwa.
Mtaalam wa masuala ya Kilimo
katika kiwanda cha Sukari cha Kagera, Bi. Salma Msonga, (kulia)
akimueleza Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe Dkt. Ashatu Kijaji
(Mb) (kushoto) hatua za kuzalisha miwa kuanzia mbegu hadi uvunaji baada
ya Naibu Waziri huyo kutembelea shamba la kiwanda hicho Mkoani Kagera
kujionea uzalishaji wa sukari kiwandani hapo.
Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Wizara ya Fedha na Mipango
………………
Benny Mwaipaja, Karagwe
NAIBU Waziri wa Fedha na Mipango,
Dkt. Ashatu Kijaji, amewataka wakulima wa miwa wanaozunguka Kiwanda cha
Sukari cha Kagera (Kagera Sugar) kuchangamkia soko la uhakika la zao
hilo kwa kuongeza uzalishaji wa miwa kutokana na uhitaji mkubwa wa miwa
kwa ajili ya uzalishaji wa miwa katika kiwanda hicho
Dkt. Kijaji alitoa wito huo baada
ya kutembelea kiwanda hicho na kuelezwa kuwa katika msimu wa kilimo cha
miwa uliopita wakulima wa miwa wanaozunguka kiwanda hicho walilipwa
Shilingi bilioni 4 baada ya kukiuzia kiwanda hicho zaidi ya tani 56,000
za miwa.
Alisema kuwa bado mahitaji ya miwa
kwa ajili ya kuzalisha sukari kiwandani hapo ni makubwa na kuwataka
wakulima hao kupitia umoja wao wa wakulima wadogo wa miwa kuhamasishana
kuongeza uzalishaji ili waweze kujikwamua kiuchumi.
Kiwanda cha Sukari cha Kagera
kimeendelea kuongeza uzalishaji tangu kipate wawekezaji ambapo
uzalishaji huo umeongezeka kutoka tani 25,000 mwaka 2011/2012 hadi
kufikia tani 75,000 na katika kipindi cha miaka mitano ijayo uzalishaji
utafikia tani 170,000.
Afisa Mwendeshaji Mkuu wa Kiwanda
hicho Bw. Ashwin Rana alisema wameanzisha Kitengo maalumu cha
kuwaendeleza wakulima wadogo wa miwa wanaozunguka mashamba yao kwa
kuendelea kuwapatia vitendeakazi ikiwemo matrekta, utaalamu pamoja na
mbegu bora za miwa ili waweze kuchangia kuzalisha miwa yatakayosaidia
waweze kufikia malengo yao ya kuongeza uzalishaji wa sukari.
Bw. Rana alisema kuwa tangu
walipoanza kuunda umoja wa wakulima wadogo wa miwa wanaozunguka mashamba
yao mwaka 2006, uzalishaji wao umeongezeka kutoka tani 0 hadi tani
56,000 ambazo kiwanda hicho kilinunua msimu uliopita na kwamba
wanatarajia uzalishaji wao utaongezeka zaidi.
“Mahitaji ya sukari nchini kwa
mwaka ni tani 450,000 lakini uzalishaji uliopo hivi sasa ni tani 320,000
na kwa mikakati ya Kiwanda cha Sukari Kagera ya kuongeza mashamba na
teknolojia ya uzalishaji wa bidhaa hiyo utapunguza kwa kiasi kikubwa
upungufu huo” aliongeza Bw. Rana.
Kaimu Kamishna wa Mamlaka ya
Mapato Tanzania TRA Bw. Beatus Nchota, alieleza kuwa Mamlaka hiyo
inapongeza jitihada kubwa ya kiwanda hicho kuongeza uzalishaji hatua
ambayo itaongeza mauzo, ajira na hatimaye kuongeza kiwango cha kodi
ambayo Kiwanda hicho kimekuwa kikilipa kwa kiwango kikubwa.
Post a Comment