PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: Rais wa TFF Atembelea Makao Makuu ya Shirikisho la Soka Barani Afrika CAF
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
Rais wa shirikisho la soka nchini Tanzania Wallace Karia pamoja na Kaimu Katibu Mkuu Kidao Wilfred wametembelea makao makuu ya shirikisho...
Rais wa TFF Watembelea Makao Makuu ya Shirikisho la Soka Barani Afrika CAF
Rais wa shirikisho la soka nchini Tanzania Wallace Karia pamoja na Kaimu Katibu Mkuu Kidao Wilfred wametembelea makao makuu ya shirikisho la soka barani Afrika CAF na kukutana na Rais Bw. Ahmad Ahmad.

Ziara hiyo ya Rais Karia imefanyika jana ambapo walitua kwenye ofisi za CAF zilizopo Cairo nchini Misri na kupokelewa na Rais Ahmad Ahmad kisha kufanya kikao kilichojadili maendeleo ya soka nchini.

Aidha kikao hicho kilihudhuriwa pia na Rais wa Heshima wa TFF ambaye ni Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya CAF, Bw. Leodegar Tenga.
Rais wa CAF ameahidi kuisaidia TFF katika mipango ya maendeleo ya soka nchini ili kuongeza umoja kwasababu soka siku zote hujenga umoja na mshikamano.

Rais Karia na wenzake waliingia madarakani August 12 mwaka huu ambapo tangu waanze majukumu yao wamekuwa wakijitahidi kuhakikisha soka linapiga hatua kwa kutafuta wadhamini ambao watawezesha maendeleo hayo ya soka.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top