Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Joseph
Magufuli, ameeleza sababu zinazomfanya achelewe kutimiza ahadi ya
milioni 50 kwa kila kijiji alizoziajidi wakati wa kampeni za kugombea
urais kuwa ni kutokana na kuwepo kwa mambo mengi nchini yanayohitaji
utekelezaji wa haraka.
Rais Magufuli ameyasema hayo leo alipokuwa akizungumza na wananchi wa
Mkoa wa Mwanza katika mkutano wa hadhara ikiwa ni moja ya vitu
alivyopanga kuvifanya katika ziara yake ya kikazi ya siku mbili mkoani
hapo.
Ameeleza kuwa ameona ni sahihi kuanza na mambo ya muhimu zaidi kama vile
miundombinu ya barabara, huduma za afya pamoja na elimu kabla ya kutoa
fedha hizo ambazo aliziahidi katika iilani ya uchaguzi wa mwaka 2015.
“Halitokuwa jambo jema mimi kutoa milioni 50 kwa kila kijiji nchini
wakati huduma mbalimbali kama vile elimu, afya na miundombinu ya
barabara na usafirishaji haijakaa vizuri. lakini niwahakikishie kuwa
hizo fedha zipo na zitakabidhiwa kwa kila kijiji kama nilivyosema,”
alisema Rais Magufuli.
“Inabidi muwe watulivu wakati serikali ikishughulikia matatizo na
changamoto zinazohitaji utatuzi wa haraka kabla hatujazitoa fedha hizo,”
aliongeza Rais Magufuli.
Rais Magufuli alimtaka pia Mkuu wa mkoa wa mwanza kuhakikisha kuwa
anachochea maendeleo ya viwanda na kupitia hivyo nchi itapata maendeleo.
“Viwanda vitatengeneza ajira nyingi kwa watanzania na vitaongeza mapato
ya serikali. Mapato yakiongezeka serikali itaweza kutoa huduma
mbalimbali kwa wananchi,” Alisema Rais.
Home
»
KITAIFA
»
Matukio
» Rais Magufuli Aeleza Sababu za Kutokugawa Milion 50 Alizoahidi Kwa Kila Kijiji
About Author
Journalist , Enterpreneur, Lecturer and Blogger. Email :ngoboleaa@gmail.com.
Advertisement
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment