Wakati majadiliano kati ya Serikali ya Tanzania na Kampuni ya Barrick
Gold Corporation kuhusu wizi unaodaiwa kufanywa kwenye uchimbaji na
usafirishaji wa mchanga wa madini (makinikia) yakiingia siku ya 64,
Ikulu imesema majadiliano hayo yanaendelea.
Majadiliano hayo yanafanyika kipindi ambacho Watanzania wengi wana shauku ya kuona rasilimali za madini zinanufaisha Taifa.
Katika majadiliano hayo yaliyoanza Julai 31, timu ya Tanzania inaongozwa
na Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Palamagamba Kabudi.
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais- Ikulu, Gerson Msigwa amesema
majadiliano yanaendelea na wananchi wasubiri wataelezwa kitakachojiri.
“Majadiliano bado yanaendelea, wakiwa tayari watasema kwani hawawezi
kuwa wanajadiliana mara wanakwenda kusema katika media," amesema Msigwa.
Mazungumzo hayo yalianza kufanyika kipindi ambacho Rais John Magufuli
alikuwa amekwishapiga marufuku ya kusafirisha nje makinikia hadi mgogoro
wa kimaslahi kati ya wawekezaji hao na Serikali utakapomalizika.
Miongoni mwa kinachojadiliwa ni kodi ambayo Mamlaka ya Mapato Tanzania
(TRA) imeitaka Kampuni ya Acacia kuilipa Serikali ya Tanzania Dola za
Marekani Bilioni 190 ambazo ni zaidi ya Sh 434 trilioni zinazodaiwa
kutokana na malimbikizo ya kodi na adhabu.
Msingi wa mazungumzo hayo ni baada ya Rais Magufuli kuunda tume mbili
kuchunguza madai ya wizi na ufisadi unaodaiwa kufanywa na wawekezaji hao
kwa zaidi ya miaka 19 iliyopita tangu walipoanza uzalishaji wa dhahabu
Home
»
HABARI ZA BIASHARA
» Majadiliano kati ya Tanzania na Kampuni ya Barrick Gold Corporation kuhusu Makinikia Bado Yanaendelea
About Author
Journalist , Enterpreneur, Lecturer and Blogger. Email :ngoboleaa@gmail.com.
Advertisement
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment