Mkuu
wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka akizugumza na wananchi wa Kata ya
Ngulyati wilayani Bariadi katika Mkutano wa hadhara wakati wa ziara yake
yenye lengo la kusikiliza kero mbalimbali za wananchi na kuzipatia
ufumbuzi.
Mchungaji
Nicholuos Chimbu mkazi wa Kijiji cha Ngulyati(kulia) wilayani Bariadi
akiwasilisha kero yake kwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony
Mtaka(hayupo pichani) alipofanya ziara wilayani humo kwa lengo la
kuzikiliza kero za wananchi na kuzitafuatia ufumbuzi.
Mkuu
wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka(kulia) na Mkuu wa Wilaya ya
Bariadi, Mhe.Festo Kiswaga wakiteta jambo wakati wa ziara ya Mkuu wa
Mkoa katika Kata ya Ngulyati aliyofanya kwa lengo la kusikiliza kero za
wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.
Minza
Maduhu mkazi wa Kijiji cha Ngulyati wilayani Bariadi akiwasilisha kero
yake kwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka(hayupo pichani)
alipofanya ziara wilayani humo kwa lengo la kuzikiliza kero za wananchi
na kuzitafuatia ufumbuzi
Eliasi
Hopi mkazi wa Kijiji cha Nyasosi Kata ya Ngulyati wilayani Bariadi
aliwasilisha kero kwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka(hayupo
pichani) alipofanya ziara wilayani humo kwa lengo la kuzikiliza kero za
wananchi na kuzitafuatia ufumbuzi.
Afisa
Uhusiano wa TANESCO Mkoa wa Simiyu akitolea ufafanuzi suala la
utekelezaji wa Mradi wa Umeme Vijijini REA Awamu ya III ambalo
liliulizwa na wananchi wa Kata ya Ngulyati wakati wa ziara ya Mkuu wa
Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka aliyoifanya kwa lengo la kusikiliza
kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.
Kikundi
cha Burudani cha Msanii Polepole kutoka Ngulyati kikitoa burudani ka
wananchi na viongozi katika ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony
Mtaka(hayupo pichani) aliyoifanya katika kata ya Ngulyati wilayani
Bariadi kwa lengo la kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia
ufumbuzi.
Na Stella Kalinga, Simiyu
Mkuu
wa Mkoa wa Simiyu,Mhe.Anthony Mtaka ametoa wito kwa wananchi Wilayani
Bariadi mkoani humo kujiunga na Mfuko wa Afya ya Jamii(CHF).
Mtaka
ametoa wito huo wakati alipokuwa akizungumza na wananchi wa Kata ya
Ngulyati wilayani Bariadi wakati wa ziara yake yenye lengo la kusikiliza
kero mbalimbali za wananchi na kuzipatia ufumbuzi.
Amesema
azma ya Serikali ni kuwa ifikapo mwaka 2020 Watanzania wote wawe
wamejiunga na Mfuko wa Afya ya Jamii(CHF) au Mfuko wa Taifa wa Bima ya
Afya (NHIF), hivyo akawahamasisha wananchi ambao bado hawajajiunga na
CHF kujiunga kwa kuwa gharama yake ni nafuu.
“Watu
wa Ngulyati ni wafanyabiashara wazuri, wafanyakazi wazuri, wakulima
wazuri ningetamani kuwaona wote hapa mnakuwa na kadi za Mfuko wa Afya ya
Jamii ambazo zinapatikana kwa gharama ya shilingi 10,000, hii ni sawa
na kuku mmoja tu mnapata matibabu watu sita kwa maana ya baba, mama na
watoto wa nne” amesema.
Ameongeza
kuwa Serikali inaendelea kuimarisha vituo vya kutolea huduma za afya
ili wananchi waweze kupata huduma bora, ambapo Serikali kupitia Mradi wa
RBF(Result Based Financing/Kulipa kulingana na Matokeo) imetoa fedha
kwa ajili ya kuboresha huduma.
Akitoa
ufafanuzi wa fedha hizo Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya Bariadi,
Ndg.Abdallah Malela amesema, kupitia mradi wa RBF Halmashauri hiyo
imepokea shilingi milioni 260, zilizogawanywa katika vituo vilivyopo 26
vya kutolea huduma za afya ambapo kila kituo kimepokea shilingi Milioni
10 ili kuboresha utoaji wa huduma za Afya.
Aidha,
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu amemtaka Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe.Festo
Kiswaga kufuatilia na kuhakikisha Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa
Bariadi anawasilisha kwake taarifa ya fedha za Mradi wa RBF alizopokea
na kazi zilizofanyika katika vituo vya kutolea huduma.
“Mhe.
DC umesikia hapa hawa watu wamepokea fedha toka mwezi saba mwaka huu na
leo ndio wamekaa kikao cha mpango, maana yake ni kwamba mwezi wa nane
wananchi hawajapata huduma zilizokusudiwa na Wizara ya Afya, na naamini
yanayofanyika kwenye kituo hiki yapo katika vituo vyako vyote, sasa
nimuombe Mkurugenzi wa Mji Jumatatu atuletee taarifa ya mpango
uliotekelezeka” amesema Mtaka.
Mkuu
wa Wilaya ya Bariadi, Mhe.Festo Kiswaga amemhakikishia Mkuu wa Mkoa wa
Simiyu kuwa atalifuatilia suala hilo pamoja na kutekeleza maelekezo yote
aliyoyatoa katika ziara hiyo na ameahidi kuwachukulia hatua watumishi
watakaoshindwa kutimiza wajibu wao katika kuwahudumia wananchi.
Kuhusu
suala la taratibu za uwekaji wa umeme wa REA awamu ya III kwa wananchi
na Taasisi za Umma ambalo liliwasilishwa na wananchi akiwemo Mwl. Daudi
Jackson, Mkuu wa Mkoa, Mhe.Anthony Mtaka amesema atakutana na Meneja wa
TANESCO Mkoa siku ya Jumatatu Septemba 04, ili wajadili namna na
kushughulikia suala hilo.
Katika
hatua nyingine Mtaka amemtaka Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya
Wilaya ya Bariadi kuhakikisha Mhandisi wa Ujenzi wa Halmashauri anafika
eneo la ujenzi wa Soko la Ngulyati Jumatatu tarehe 04 Septemba kukutana
na viongozi wa Kijiji na Kata, kwa ajili ya kuanza mpango wa ujenzi wa
soko hilo ili kutatua kero ya ukosefu wa soko na kuwawezesha wananchi
kupata sehemu ya kuuzia bidhaa zao.
Wakati
huo huo Mtaka amewataka wananchi kutumia vizuri msimu wa kilimo, kulima
mazao yanayostahimili ukame na akawasisitiza kutunza chakula
walichokipata katika msimu uliopita kwasababu Serikali haitakuwa na
chakula cha msaada.
Post a Comment