Meneja kiongozi wa NSSF mkoa wa Arusha kushoto Dr. Frank Maduga akizungumza na waandishi wa habari juu ya kuwapeleka waajiri 126 mahakamani kwa kosa la kutowasilisha michango ya waajiriwa inayofikia kiasi cha shilingi bilioni moja nukta tano kwa kipindi cha miezi sita sasa. |
NA: ANDREA NGOBOLE, PMT
Jumla ya Kampuni
126 zinazodaiwa kiasi cha shilingi bilioni moja pointi tano zinatarajiwa
kufikishwa mahakamani wiki ijayo na shirika la Taifa la hifadhi ya jamii NSSF
mkoani Arusha kwa kosa la kutowasilisha michango ya wafanyakazi wao kwa kipindi
cha miezi sita iliyopita.
Akizungumza
na waandishi wa habari ofisini kwake mapema jana meneja kiongozi wa NSSF mkoani
Arusha Dr. Frank Maduga amesema kuwa makampuni hayo yamegawanyika kati ya
waajiri wakubwa 14 wanaolipia kiasi cha shilingi milioni 50 na kuendelea, wajiri wa kati 69 wanaolipia
milioni 5 hadi 49.9 na wale waajiri wadogo 53 wanaolipia kiasi cha shilingi
elfu ishirini hadi milioni 4.9 kwa mwezi ambapo jumla ya michango yao
inafikia Zaidi ya bilioni moja nukta tano mpaka sasa.
“Waajiri
wakubwa wote wamekwisha pelekewa onyo la Mwisho na sasa taratibu za kimahakama
zinaendelea hivyo kuanzia jumatatu ya tarehe 2 october 2017 mtawajua ni waajiri
gani wameshindwa kutekeleza wajibu wao na kwa kiasi gani wanadaiwa kila mmoja
wao” alisema dokta Maduga
Amesema kuwa
Mashitaka yatakayokuwa yakiwakabali waajiri hao ni kutowasilisha michango ya
wafanyakazi wao kwa wakati na kwa muda unaozidi miezi sita, kitendo hicho
kimekuwa na madhara makubwa kwa wafanyakazi na wategemezi wao kwa kukosa huduma
za matibabu , fao la uzazi na pia kuna baadhi ya wanachama taarifa zao za
kumbukumbu hazioneshi fedha yoyote katika muda ule ambao michango
haijawasilishwa na kusababisha taharuki na msongo wa mawazo kwa wafanyakazi
husika.
Aidha Meneja huyo amewatakata Wafanyakazi kujenga tabia ya kufuatilia iwapo michango yao inawasilisha au la na kwa kufika katika ofisi za NSSF na kufanya uhakikiki ili kupunguza malalamiko pindi watakapohitaji mafao yao
Aidha Meneja huyo amewatakata Wafanyakazi kujenga tabia ya kufuatilia iwapo michango yao inawasilisha au la na kwa kufika katika ofisi za NSSF na kufanya uhakikiki ili kupunguza malalamiko pindi watakapohitaji mafao yao
Mwanachama
ana haki ya kulipwa michango yake yote akiacha kazi au kampuni ikifa na kuacha
kuendesha biashara hulazimika kulipa fedha zote za michango ya wanachama na wao
kama taasisi inayosimamia haki za waajiriwa huhakikisha malipo yote yanalipwa
na kutolea mfano kampuni za snowcrest na mukidoma zilizositisha shughuli zake
na kutangaza kufilisika walihakikisha
kuwa kila mfanyakazi anapata mafao yake bila wasiwasi wowote.
Amesisitiza
kuwa mwanachama akishaacha kazi atasubiri kwa kipindi cha miezi sita ndiyo
aweze kupewa fao la kustaafu na kipindi hiki huwekwa ili kumpa nafasi
mwanachama kuweza kutafuta kazi na ama kuajiriwa na kampuni nyingine na
changamoto inayowakabili ni kuwa baadhi ya wanachama hufoji barua za kuacha
kazi ili waweze kupewa mafao yao huku bado wanafantya kazi jambo ambalo halikubaliki
kwa mwanachama kulipwa fao lake huku anafanya kazi.
Maduga amesema kuwa kutakua na mkutano mkuu wa Mfuko huo utakaofanyika mwaka huu hapa jijini Arusha katika ukumbi wa kimataifa wa mikutano wa Arusha AICC na mgeni rasmi anayetarajiwa kufungua mkutano huo ni waziri mkuu Kassimu Majaliwa ambapo wadau mbalimbali watakutana kujadili maendeleo pamoja na changamoto za mfuko huo
Maduga amesema kuwa kutakua na mkutano mkuu wa Mfuko huo utakaofanyika mwaka huu hapa jijini Arusha katika ukumbi wa kimataifa wa mikutano wa Arusha AICC na mgeni rasmi anayetarajiwa kufungua mkutano huo ni waziri mkuu Kassimu Majaliwa ambapo wadau mbalimbali watakutana kujadili maendeleo pamoja na changamoto za mfuko huo
Naye Straton
Simon Afisa msimamizi wa fao la matibabu NSSF kanda ya kaskazini inayowakilisha mikoa
ya ARUSHA,KILIMANJARO, TANGA na MANYARA amesema kuwa fao la matibabu hutolewa
bure na mfuko huo kwa kila mwanachama anayekuwa amewekewa michango yake kwa
miezi mitatu na kuendelea na fao hili
halihusiani na kukatwa akiba yako siku utakayostafu kazi au kampuni yako
kusimama kufanya kazi hivyo amewataka wanachama wasiwe waoga kutumia fao hili kwani lina
faida kwa mwanachama na wategemezi wake wane ambao ni mke au mume na watoto
wane.
Straton Simon amesema kuwa mfuko huo umeboresha fao la uzazi ambalo litawawezesha kinamama kupata matibabu bure kabla ya kujifungua na baada ya kujifungua ili kuboresha afya ya mama na mtoto
Straton Simon amesema kuwa mfuko huo umeboresha fao la uzazi ambalo litawawezesha kinamama kupata matibabu bure kabla ya kujifungua na baada ya kujifungua ili kuboresha afya ya mama na mtoto
Amesema kwa
Arusha pekee NSSF ina mkataba wa matibabu kwa wanchama wake na hospitali 34
zinazotibu wanachama wote wa hiari na wale waajiriwa ambao mpaka sasa wanafikia
18,400 na kwa kanda nzima ya kaskazini
wanafikia wanachama 34000 wanaopata fao hilo la matibabu na kuwasihi wanachama
wengine wote wahakikishe wanajaza fomu na kuchagua moja ya hospital ambayo
ungependa kutibiwa kati ya hizo hospitali 34 ili wanufaike na fao hilo muhimu kwa maisha ya mwanachama.
Post a Comment