PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: MKURUGENZI JIJI LA ARUSHA AWATAKA VIONGOZI WA MTAA KILA IJUMAA IWE SIKU MAALUM KUSIKILIZA NA KUTATUA KERO ZA WAKAZI
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
Watendaji wa mitaa pamoja na Mkurugenzi wa jiji la Arusha Katika Kikao maalum cha utendaji kazi Watendaji wakiwa wakimsikiliza mkurug...
Watendaji wa mitaa pamoja na Mkurugenzi wa jiji la Arusha Katika Kikao maalum cha utendaji kazi
Watendaji wakiwa wakimsikiliza mkurugenzi wa jiji
Watendaji wa kata pamoja na mitaa katika halmashauri ya  jiji la Arusha wameagizwa kutenga siku malum katika wiki kwa ajili ya Kusikiliza malalamiko ya wananchi na kuyapatia utatuzi kwa kuwa mengine yako ndani ya uwezo wao kiutendaji.

Akizungumza na watendaji wote wa Mitaa katika jiji la Arusha Mkurugenzi  Bwana Athumani Kihamia amesema kuwa amewapa watendaji hao kila siku ya ijumaa ya kila wiki kuhakikisha wanaiweka kwa ajili ya kusikiliza malalamiko ya wananchi na kuyajibu kwa maandishi .

Kihamia amesema kuwa mara nyingi kumekuwa na malalamiko mengi yanapelekwa kwa mkuu wa mkoa ,Mkuu wa wilaya ,na Mkurugenzi pamoja na ofisi za juu ambayo yana uwezo wa kutatuliwa katika ngazi za mitaa ambayo ni kazi ya watendaji hao.

Naye Bwana Kihamia amesema kuwa ametenga siku ya jumatano kwa ajili ya kusikiliza malalamiko ya wananchi na kuyapatia utatuzi ili kuwapunguzia wananchi matatizo ambayo yanauwezo kutatuliwa kwa wakati.


“Mpaka wale watu wanafika huku wanaweka foleni kwa mkurugenzi ,mkuu wa wilaya au mkuu wa mkoa nataka mje tu siku moja mtembelee muone matatizo wanayoyasema yako ndani ya uwezo wenu watendaji na ikiwezekana muweke tangazo ili wananchi wajue siku hiyo iwe maalum” Mkurugenzi Amesema Kihamia

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top