PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: Bulembo Awasilisha Barua ya Kutogombea Nafasi ya Uenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
  Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi wa Chama cha Mapinduzi(CCM), Alhaj Abdallah Bulembo amewasilisha barua kwa Katibu Mkuu wa CCM kut...
Bulembo Awasilisha Barua ya Kutogombea Nafasi ya Uenyekiti  wa Jumuiya ya Wazazi
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi wa Chama cha Mapinduzi(CCM), Alhaj Abdallah Bulembo amewasilisha barua kwa Katibu Mkuu wa CCM kutogombea nafasi ya uenyekiti wa jumuiya hiyo.

Bulembo aliwahi kusema kuwa hatogombea tena lakini baadaye aliamua kuchukua fomu. Hata hivyo Bulembo amesema aliamua kuchukua fomu ya kugombea baada ya kupata shinikizo kutoka kwa makatibu wakuu na wazee wa jumuiya hiyo.

"Sasa leo(Jumanne) nimewaita kuwaeleza sitagombea tena licha ya kuchukua fomu, naamini wagombea 48 waliopatikana, kuna mmoja atatufaa kuongoza jumuiya hii, leo ninapeleka barua kwa katibu mkuu wa chama (Abdulrahiman Kinana) ya kumweleza dhamira yangu hii,” amesema Bulembo leo Jumanne alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini hapa.

Bulembo amesema uchaguzi katika ngazi ya Taifa utafanyika kuanzia Novemba 20 hadi 23, wagombea wote wapo lakini yeyote aliyeanza kampeni mapema huyo ameshajikata," amesema.

Kuhusu hoja ya kuchukua fomu amesema haikuwa dhambi kwa kuwa kanuni za chama zinaruhusu na upo uwezekano wa kuwa na nafasi mbili za uongozi.

"Kumekuwa na upotoshaji kwamba, ukiwa mbunge au waziri hauwezi kugombea nafasi nyingine, sasa hapa nina kitabu cha kanuni za mwaka 2005, 2010, 2012 na 2017 zinasema kiongozi au mbunge, waziri anaweza kugombea ila kamati kuu ya chama itaamua inavyofaa, kama bado anahitajika atapitishwa lakini mie sitagombea tena,” amesema.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top