PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: Maalim Seif Amjulia hali Hospital Tundu Lissu Nairobi Kenya
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi CUF, Mhe. Seif Sharif Hamad leo Septemba 26, 2017 ameingia jijini Nairobi Kenya kwenda kumjuli...

Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi CUF, Mhe. Seif Sharif Hamad leo Septemba 26, 2017 ameingia jijini Nairobi Kenya kwenda kumjulia hali Mbunge wa Singida Mashariki na Rais wa Chama Cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Tundu Lissu ambaye alipigwa risasi.
Mwenyekiti wa kamati ya muda ya uongozi CUF, Julius Mtatiro amethibitisha hilo na kusema kuwa kiongozi huyo na baadhi ya viongozi wa CUF wamewasili nchini Kenya kwa ajili ya kwenda kumuona Tundu Lissu.

"Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi CUF, Mhe. Seif Sharif Hamad ameingia jijini Nairobi kumjulia hali Mbunge wa Singida Mashariki na Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika Mhe. Tundu Antipas Lisu (leo) ambaye amelazwa Hospitali ya Nairobi" alisema Julius Mtatiro

Mhe. Shariff Hamad ameongozana na Mhe. Juma Duni Haji Nairobi kumjulia hali, Mhe Tundu Lissu.

Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu alishambuliwa kwa risasi na watu wasiojulikana Septemba 7, 2017 mjini Dodoma na kisha baadaye kupelekwa nchini Kenya kwa matibabu zaidi.
 

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top