Dar es
Salaam;WAZIRI wa Maliasili na Utalii Prof Jumanne Maghembe mwishoni mwa
wiki hii alizindua rasmi usajili wa msimu wa nane wa mbio za Rock City
Marathon huku akiahidi kushirikiana na waandaaji wa mbio hizo katika
kuhakikisha kuwa zinatumika vema kuutangaza utalii wa ndani.
Akizungumza
kwenye hafla fupi ya uzinduzi huo iliyofanyika katika Hoteli ya Serena
jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa mchezo huo
wakiwemo viongozi wa serikali pamoja na wadhamini mbalimbali wa mbio
hizo, Waziri Maghembe alisema azma yake hiyo inasukumwa na malengo ya
mbio hizo ambayo ni kutumia mchezo wa riadha katika kutangaza utalii
hususani katika Ukanda wa Ziwa.
"Kwa
kuzingatia uzito wa malengo ya mbio hizo nitamke bayana kuwa nipo tayari
kushirikiana na waandaaji wa mbio hizi kuhakikisha kwamba kuanzia mwaka
huu mbio hizi zinafana na zinavutia washiriki wengi zaidi hususani wa
kimataifa,'' alisema Waziri Maghembe ambae pia alithibitisha ushiriki
wake kwenye mbio hizo zinazoratarajiwa kufanyika Octoba 29, mwaka huu
kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza na kupita katika barabara
mbalimbali za jiji hilo kabla hazijamalizikia katika uwanja huo.
Mbali
na ushiriki wake,Waziri Maghembe alitoa wito kwa mashirika mbalimbali
yaliyo chini ya wizara yake ikiwemo la Hifadhi za Taifa(Tanapa), Mamlaka
ya Usimamizi Wanyamapori (TAWA), Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro
(NCAA), Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) na Makumbusho ya Taifa
kuhakikisha wanashiriki kikamilifu katika kufanikisha mbio hizo.
"Ukanda
wa Ziwa una vivutio vingi ambavyo pia kama Wizara yenye dhamana ya
utalii lazima tuvigeukie na kuvitangaza kwa nguvu na kwa njia tofauti
ikiwemo michezo,'' alisema Waziri Maghembe huku akivitaja baadhi ya
vivutio hivyo kuwa ni pamoja na Kisiwa cha Saanane, Makumbusho ya kabila
la Wasukuma pamoja na tamaduni za makabila ya wakazi wa Kanda ya Ziwa.
Mbio
za Rock City Marathon zilizoanzishwa miaka minane iliyopita zinazozidi
kujiongezea umaarufu kila mwaka na tayari zimefanikiwa kuwavutia baadhi
ya wadhamini ikiwa ni pamoja na kampuni za TIPER, PUMA, Bodi ya Utalii
Tanzania (TTB),Mwanza Hotel , Real PR Solutions Limited, Afrimax
Strategic Partnerships Limited, EF Outdoor, CF Hospital na ATCL.
Kwa
upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya mbio hizo, Bw Zenno
Ngowi alitoa wito kwa washiriki wa ndani hususani wa mikoa ya Kanda ya
Ziwa pamoja na wadhamini kujitokeza kwa wingi kushiriki katika mbio hizo
ambazo kwa mwaka jana zilifanikiwa kuhusisha washiriki zaidi ya 2000 na
watazamaji zaidi ya 30,000.
Naye
Mratibu wa mbio hizo zinazoandaliwa na kampuni ya Capital Plus
International, Bi Adeline Ndesanjo alisema mbio za mwaka huu
zinatarajiwa kuhusisha washiriki wengi zaidi kutoka kila kona ya dunia
ikiwemo Afrika, Ulaya,China,Mashariki ya Kati hususani Israel na
Marekani huku akitoa wito kwa washiriki wa ndani kujisajili kwa wingi
ili kuthibitisha ushiriki wao kwenye mbio hizo.
Akizungumza
kwa niaba ya wadhamini wengine wa mbio hizo Meneja Masoko wa Kampuni ya
mafuta ya Puma, Bw Machumani Shebe alisema ushiriki wao umechagizwa
zaidi na azma ya kampuni hiyo kuisaidia serikali katika kuutangaza
utalii wa ndani.
"Tukiwa
kama wadau muhimu katika biashara ya mafuta hususani mafuta ya ndege
tunategemea sana ustawi wa sekta ya utalii katika kuongeza soko la
biashara yetu na kwa kuwa mchezo wa riadha umekuwa ukitumika zaidi
katika kuwavutia watalii tukaona kuna haja ya kuunga mkono ufanikishaji
wa mbio hizi,'' alisema.
WAZIRI
wa Maliasili na Utalii Prof Jumanne Maghembe akizungumza na wadau
mbalimbali wa mchezo wa riadha hapa nchini pamoja na waandaaji wa mbio
za Rock City Marathon kwenye hafla maalumu ya uzinduzi rasmi usajili wa
msimu msimu wa nane wa mbio hizo iliyofanyika mwishoni mwa wiki jijini
Dar es salaam.
Mwenyekiti
wa Kamati ya Maandalizi ya mbio hizo, Bw Zenno Ngowi akizungumza kwenye
hafla hiyo. Alitoa wito kwa washiriki wa ndani hususani wa mikoa ya
Kanda ya Ziwa pamoja na wadhamini kujitokeza kwa wingi kushiriki katika
mbio hizo ambazo kwa mwaka jana zilifanikiwa kuhusisha washiriki zaidi
ya 2000 na watazamaji zaidi ya 30,000.
Mratibu
wa mbio hizo zinazoandaliwa na kampuni ya Capital Plus International,
Bi Adeline Ndesanjo akitoa maelezo kuhusu maandalizi ya mbio hizo kwenye
hafla hiyo. Alisema mbio za mwaka huu zinatarajiwa kuhusisha washiriki
wengi zaidi kutoka kila kona ya dunia ikiwemo Afrika,
Ulaya,China,Mashariki ya Kati hususani Israel na Marekani .
Wadhamini
nao hawakuwa nyuma!Meneja Masoko wa Kampuni ya mafuta ya Puma Energy,
Bw Machumani Shebe alisema ushiriki wao kwenye mbio hizo umechagizwa
zaidi na azma ya kampuni yake hiyo kuisaidia serikali katika kuutangaza
utalii wa ndani.
Baadhi ya wageni waalikwa waliohudhuria hafla hiyo.
WAZIRI
wa Maliasili na Utalii Prof Jumanne Maghembe akiwa kwenye picha ya
pamoja na waandaaji wa mbio hizo pamoja na wadau mbalimbali wa mchezo
huo wakiwemo viongozi wa serikali pamoja na wadhamini wa mbio hizo.
Post a Comment