Mkurugenzi wa shule ya Upendo Friends Isabella Mwampamba (Watatu kulia) akikabidhi msaada katika shule ya msingi Meru Kitengo Maalumu kilichopo wilaya ya Arusha Mjini.Picha na Ferdinand Shayo |
Mkurugenzi wa shule ya Upendo Friends Isabella Mwampamba akikabidhi msaada katika shule ya msingi Meru Kitengo Maalumu kilichopo wilaya ya Arusha Mjini.Picha na Ferdinand Shayo |

Na Ferdinand
Shayo,Arusha.
Shule ya
Msingi ya Upendo Friends imesaidia kitengo Maalumu cha Watoto wenye mahitaji
maalumu wakiwemo walemavu wasiosikia na kuona ikiwa ni njia mojawapo ya kuunga
mkono juhudi za serekali katika kuboresha elimu kwa watoto wenye ulemavu.
Mkurugenzi
Mkuu wa Shule hiyo Isabella Mwampamba alisema kuwa wamefika katika kitengo cha
watoto wenye uhitaji maalumu kilichopo katika shule ya Msingi Meru na kutoa
misaada ya chakula pamoja na vifaa vya michezo.
Isabella alisema
kuwa ni wajibu wa wanajamii kuhakikisha kuwa wanawasaidia watoto wenye uhitaji
kwa kuboresha mazingira ya kujifunzia na miundombinu rafiki kwa watoto wenye
ulemavu.
Kaimu Afisa
Elimu shule ya Msingi Wilaya ya Arusha
Mjini Eunice Tondi alisema kuwa serikali imeendelea kuwekeza
kwenye elimu ya watoto wenye ulemavu kwa kuongeza vifaa vya kisasa kwa watoto
wasiona ili waweze kufanya vizuri kitaaluma.
“Kwa
kushirikiana na wadau wa maendeleo serikali imeongeza nguvu na kuboresha
vitengo vya watoto wenye ulemavu ili waweze kupata elimu bora na kujikwamua
kimaisha “ Alisema
Mkuu wa
Shule ya Msingi Meru Musa Luambano ameshukuru shule ya Upendo Friends kwa
kujitolea kusaidia shule hiyo na kuhakikisha kuwa wanafunzi wanapata chakula
ili waweze kuhudhuria darasani vizuri pia amezitaka shule nyingine binafsi
kuelekeza nguvu katika kusaidia vitengo maalumu.
Post a Comment