PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: BAADA YA KUSHINDA VIKOMBE MUHIMU ZIDANE APEWA MKATABA WA MIAKA MITATU KUKINOA KIKOSI CHA REAL MADRID
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
    Mkufunzi mkuu wa Real Madrid Zinedine Zidane ameafikiana na mabingwa hao wa Ulaya na Uhispania kuhusu mkataba mpya wa miaka m...


Mkufunzi mkuu wa Real Madrid Apata mkataba mpya wa Miaka Mitatu Katika Timu Hiyo
Mkufunzi mkuu wa Real Madrid Zinedine Zidane ameafikiana na mabingwa hao wa Ulaya na Uhispania kuhusu mkataba mpya wa miaka mitatu.
Kiungo huyo wa kati wa zamani wa Real, katika miezi 18 ambayo amekuwa kwenye usukani, ameshinda Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya mara mbili na taji la La Liga mara mbili.

Akiongea mkesha wa mechi ya kwanza ya mkondo wa kwanza ya Super Cup ya Uhispania itakayochezewa Barcelona, alisema: "Hadithi yangu na Real Madrid ni zaidi ya mikataba na saini.
"Nina furaha kubwa kuhusishwa na klabu hii. Lakini mkataba hauna maana yoyote."

Mchezaji huyo wa zamani wa timu ya taifa ya Ufaransa mwenye miaka 45 alikuwa mkufunzi wa Timu B ya Real kabla ya kuchukua nafasi ya Rafael Benitez Januari 2016.

Aliongeza: "Unaweza kutia saini mkataba wa miaka 10, 20. Najua niko wapi na nataka kufanya nini.
"Katika mwaka mmoja, pengine sitakuwa hapa. Mimi na Real Madrid hatutajibizana, daima.."

Real watacheza dhidi ya Barca Jumapili mechi itakayoanza saa 21:00 BST (saa tano usiku Afrika Mashariki). Mechi ya marudiano itachezewa Bernabeu Jumatano saa 22:00 BST (Saa sita Afrika Mashariki)

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top