Askofu Mteule Mchungaji Blastone Tuluwene Gavile (kushoto) akiwa
na Msaidizi wa Askofu Mteule Mchungaji Himid
John Sagga.
IBADA ya
kuwekwa wakfu kwa Askofu Mteule wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania
(KKKT) Dayosisi ya Iringa, Mchungaji Blaston Tuluwene Gavile, inatarajiwa
kufanyika Jumapili Juni 25, 2017 mjini Iringa.
Ibada
hiyo, ambayo itaambatana na kuingizwa kazini kwa Msaidizi wa Askofu, Mchungaji
Himid Sagga, itafanyika ikiandika historia kwenye Dayosisi hiyo ambapo Askofu
Mteule Gavile anachukua nafasi ya Askofu Dkt. Owdenberg Moses Mdegela ambaye
amestaafu.
Katibu
Mkuu wa KKKT Dayosisi ya Iringa, Nayman Chavalla, amesema tukio hilo maalum ni
la pili katika historia ya Dayosisi hiyo, kwani Mchungaji Gavile anakuwa ndiye
askofu wa pili tangu kuanzishwa kwake.
Aidha,
katika ibada hiyo Askofu Mteule Blaston Gavile atamuingiza kazini Msaidi wake
Mchungaji Himid John Sagga.
Awali
akielezea jinsi ibada hiyo itakavyokuwa, Chavalla alisema itaanza kwa
maandamano ya Wachungaji na washarika kutoka Usharika wa Kanisa Kuu Iringa
Mjini mpaka viwanja vya Gangilonga ambako ndiko ibada hiyo itafanyika.
"Ibada
hiyo inatarajiwa kuongozwa na Mkuu wa KKKT, Askofu Fredrick Shoo akisaidana na
Baba Askofu Mstaafu Dkt. Mdegella," alisema.
Pia katika
ibada hiyo viongozi wa Makanisa mbalimbali hapa nchini na nje ya nchi,
Wawakilishi wa vyama vya Kimisionari, Viongozi wa Kiserikali, vyama vya siasa, wageni kutoka
nchi mbalimbali, wawakilishi wa makampuni na mashirika mbalimbali watahudhuria.
Katibu
Mkuu alitoa wito kwa jamii na Wakristo wote kuendelea kuliombea jambo hilo.
Alimalizia
kwa kusema ibada inatarajia kuanza kwa maandamanao yatakayoanza saa mbili
kamili asubuhi.
MUNGU AIENDELEE
KUIBARIKI DAYOSISI YA IRINGA NA TAIFA KWA UJUMLA
Post a Comment