Rais John Magufuli amesema anajivunia kuwa na mitandao mingi ya simu ambayo inamsaidia kuwasiliana bila kero wakati wowote.
Amesema hayo jana Juni Mosi, wakati wa uzinduzi wa mfumo wa ulipaji kodi kwa njia ya kielektroniki.
“Mimi nina mitandao yote ya simu, nina Tigo, Airtel, Vodacom na hata
TTCL, mtu akinitafuta huku Airtel,akanikosa ninaweza kuweka Tigo, ili
mradi ninatambalika kila mahali,” amesema
Pia amesema, mitandao hiyo ya simu inamsaidia kupata taarifa mbalimbali zinazoendelea nchini na duniani.
Hata hivyo, Rais amezitaka kampuni za simu kuhakikisha zinalipa kodi ili serikali isikose mapato yake.
Pia Rais amesema hataki kuona taasisi nyingine zinajenga vituo vya
ukusanyaji taarifa (Data centre)na badala yake fedha hizo zitumike kwa
ajili ya shughuli nyingine za maendeleo.
“Data Centre kama hii ni mkombozi mwingine wa kupunguza kero
mbalimbali, kwa sababu ukijaza vocha yako uko Zanzibar, ukinunulia vocha
yako Kigoma au Moshi, hiyo pesa inakuja TRA, hakuna mabishano” amesema
Rais amesema hayo leo Juni Mosi, wakati wa uzinduzi wa mfumowa wa
serikali wa ulipaji kodi kwa njia ya kielektroniki ambako pia
alitembelea kituo hicho cha ukusanyaji taarifa.
Amesema chombo hicho kina faida yake na hivyo akawaomba watanzania,
wawekezaji na wafanyabiashara kukitumia chombo hicho kwa manufaa ya
taifa zima.
Post a Comment