Waziri Mkuu aliyejiuzuru kwa kashfa ya kampuni ya Richmond na Mjumbe wa
Kamati Kuu ya Chadema, Edward Lowassa amewataka watanzania kumuacha Rais
Dkt. Magufuli kuendelea kupitisha fagio sehemu mbalimbali kwani nchi
ilipokuwa imefikia ni pabaya.
Lowassa amesema kuwa ni kweli kuna baadhi ya mambo anakosea lakini si
wakati wake kumkosoa kwa sasa hivyo watanzania wanatakiwa wamuunge mkono
kwa kile anachokifanya kwakuwa anafanya kwa maslahi ya Taifa.
“Rais Magufuli ameanza vizuri kwa kubana baadhi ya mambo ambayo hayakuwa
ya msingi, kuna mambo mazuri sana mengi ameyafanya mapaka dakika hii,
lakini mwalimu Nyerere alishawahi kusema kuwa wakati unafagia ni lazima
uwe makini kwani unaweza kufagia hata shilingi, na sasa Rais Magufuli
anafagia shilingi nyingi, kwasasa tumuache afanye kazi yake lakini
tutamhukumu muda ukifika,”amesema Lowassa.
Post a Comment