PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: Kimenukaa..Zile Sauti za Kimahaba Mtandaoni za Wema na Mbowe..Kumbe Mchezo Mzima Hivi Ndivyo Ilivyokuwa A- Z..!!!
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
Siku chache baada ya kusambaa kwa sauti katika mitandao ya kijamii, ikiwemo WhatApp na Facebook, inayodaiwa kutengenezwa kwa lengo ...

Siku chache baada ya kusambaa kwa sauti katika mitandao ya kijamii, ikiwemo WhatApp na Facebook, inayodaiwa kutengenezwa kwa lengo la kumchafua Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe na mrembo wa Tanzania mwaka 2006, Wema Sepetu, hatimaye ‘dude’ limeamka na sasa kimenuka.

HAPA NDIPO ILIPOANZIA

Mwishoni mwa wiki iliyopita, sauti iliyorekodiwa kama ya watu wanaoongea kwenye simu, zilianza kusambaa kwa kasi mitandaoni, ambazo kwa kuzisikia harakaharaka, zilionekana kufanana na watu hao wawili, zikisikika kama za watu waliokuwa katika uhusiano.

Wakati sauti hizo zinasambaa, muda mchache baadaye, majibizano ya meseji kwenye simu yakaanza kusambaa pia, ambayo nayo yanahisiwa kuwa yalitengenezwa, yakiwahusisha viongozi wawili wa ngazi za juu katika Mikoa ya Arusha na Dar es Salaam, wakipongezana kwa kukamilika vizuri kwa kazi hiyo (ya kutenegeneza na kusambaza sauti). Katika majibizano hayo ya meseji za simu, ‘viongozi’ hao wawili walimsifu mtu waliyemwita Steve (anadhaniwa kuwa Steve Nyerere) kwa kuifanya kazi hiyo vizuri (ya kuigiza sauti ya kiongozi huyo).

RISASI LAWASAKA WAHUSIKA

Ili kupata mkanda kamili wa ishu hiyo, Risasi Mchanganyiko liliingia mtaani na kuifanyia kazi ili liweze kuwapa wasomaji wake kitu cha kueleweka. Freeman Alkael Mbowe ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chadema Taifa, hakupokea simu aliyopigiwa, lakini wakati Risasi Mchanganyiko likienda mitamboni, alisikika kupitia kituo kimoja cha redio jijini Arusha, akiikana sauti hiyo na kusisitiza kuwa hajawahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na muigizaji huyo na kwamba kinachofanyika ni siasa chafu, kitu ambacho kitashughulikiwa na chama.

Wema Sepetu naye simu yake iliita bila kupokelewa na hata baada ya kutumiwa ujumbe mfupi, hakujibu licha ya kuonekana kuwa umepokelewa na kusomwa.

HUYU HAPA MLEZI WA WEMA CHADEMA

Hata hivyo, Risasi Mchanganyiko lilifanikiwa kumpata mtu aliyepewa jukumu la kumlea Wema ndani ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Boniphace Jacob ambaye pia ni Meya wa Ubungo jijini Dar es Salaam na hapa anafunguka kuhusu ishu hiyo; “Tumeshaongea na wanasheria juu ya hatua kali za kisheria, kuwachukulia hatua

wote wanaoigiza sauti za viongozi wetu na kuzitumia vibaya kwa nia ya kuwadhalilisha na kuwashushia heshima, pamoja na kutoa taarifa kwenye vyombo vya dola juu ya uchunguzi ufanyike kubaini sehemu na watu wanaofanya “voice studio” kwa lengo ovu.

“Pili tumemtia moyo kamanda wetu Wema kuwa asihofu na siasa za majitaka na kwamba yote yanafanyika na wapinzani wetu, kwa sababu wanamuhofia na kumuogopa

juu ya namna anavyofanya mikakati ya kufuta

“UTUMWA WA WASANII KWA CCM”

kazi ambayo ameifanya na mpaka sasa ameandaa ujio wa wasanii wakubwa 20 ndiyo maana wanataka kumuondoa nje ya agenda yake.”

STEVE NYERERE NAYE AFUNGUKA

Steve Nyerere ambaye kwa mujibu wa meseji zilizoenezwa mtandaoni alionekana kama ndiye aliyeshughulika kutengeneza sauti hiyo ya kiume, aliruka kimanga kuhusika na suala hilo, aliloliita la kijinga na kipumbavu. “Mimi sihusiki, sikutengeneza ile sauti kwa vile sina sababu ya kufanya hivyo,

hicho ndicho ninachoweza kukuambia ila kwa nyongeza tu, niwatake Watanzania waachane na kufuatilia mambo ya kijinga na kipumbavu, tuna vitu vingi sana vya kufanya badala ya kukuza vitu kama hivi.”

SASHA NAYE AZUNGUMZIA ‘SAUTI YAKE’

Sasha, msanii ambaye hutumika kama video queen kwenye nyimbo mbalimbali za Bongo Fleva, ambaye

amefanana sauti kwa kiasi kikubwa na Wema Sepetu, anahusishwa kutumika kutengeneza sauti ya kumuigiza malkia huyo wa filamu Bongo. “Nimetumika kuiga sauti ya Wema? Hapana, sijawahi kupigiwa simu na mtu yeyote na wala sijafanya kitu kama hicho, nikuambie ukweli kuwa hili jambo ndiyo kwanza wewe unaniambia, sijui kabisa,” alisema msanii huyo.

TUNDU LISU ABEZA

Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lisu ambaye pia ni Mbunge wa Singida Mashariki, alipotakiwa kulizungumzia suala hilo, alisema ni propaganda dhaifu, zilizolenga kumchafua mwenyekiti wao, ambayo imeshindwa. “Lengo lao lilikuwa ni kumchafua mwenyekiti wetu, lakini hawajaweza kwa sababu hawezi kuchafuka kwa staili hii. Tunajua hili jambo hata tukilipeleka polisi ni kama kujisumbua tu, hawana historia ya kushughulikia shida za wapinzani.”

HAWA HAPA POLISI MAKOSA YA MTANDAO.

Risasi Mchanganyiko lilimpata mmoja wa maofisa wa kitengo cha makosa ya mtandao, ambaye alijitambulisha kwa jina moja la Fadhil, akisema yeye siyo msemaji wa suala hilo. “Ila ninachoweza kukusaidia kwa hili ni kwamba Cyber Crime haifanyi kazi pasipo kupokea malalamiko. Hao ambao sauti zao unasema zimeigwa, wanatakiwa waje kulalamika hapa na hapo ndipo polisi watakapoanza kufuatilia suala hilo. “Lakini kama wenyewe watakaa kimya bila kulalamika, basi suala hilo litaishia kama lilivyo, endapo watakuja suala hilo litafanyiwa kazi mara moja,” alisema.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top