Waziri
wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), pamoja na Naibu
wake Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), pamoja na Naibu Waziri wa Elimu
Sayansi na Teknolojia Mhe. Mhandisi Stella Manyanya (Mb), wakiwa katika
picha ya pamoja na wanafunzi wa Chuo cha Ualimu Bustani kilichoko
wilayani Kondoa mkoani Dodoma, walipotembelea bungeni mjini Dodoma, siku
ambayo Bunge limepitisha kwa kishindo Bajeti ya Sh. trilioni 31.7 kwa
Mwaka wa Fedha 2017/2018.
Katibu
Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango na Mlipaji Mkuu wa Serikali Bw. Doto
James (wa nne kulia-mbele), akiongoza Vongozi waandamizi wa Wizara ya
Fedha na Mipango kufuatilia tukio la Wabunge wakipiga kura kupitisha
Bajeti Kuu ya Serikali ya shilingi trilioni 31.7, Bungeni Mjini Dodoma.
Mbunge
wa Jimbo la Chakwa-Zanzibar, Mhe. Bhagwanji Meisuria (katikati), na
mkewe Kissum Biin Bhagwanji Meisuria, wakimpongeza Waziri wa Fedha na
Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), baada ya Bunge kupitisha
kwa kishindo Bajeti Kuu ya Serikali ya shilingi trilioni 31.7, mjini
Dodoma.
Mbunge
wa Jimbo la Misungwi, Mhe. Charles Kitwanga akimkumbatia kwa furaha na
bashasha Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb), kwa
kufanikisha kuandaa na hatimaye kupitishwa kwa Bajeti ya kihistoria ya
shilingi trilioni 31.7 ya Mwaka wa Fedha 2017/2018, mjini Dodoma.
Mbunge
wa Jimbo la Mtama, Mhe. Nape Mnauye akimpongeza Waziri wa Fedha na
Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), kwa kufanikisha kuandaa na
hatimaye kupitishwa kwa Bajeti ya kihistoria ya shilingi trilioni 31.7
ya Mwaka wa Fedha 2017/2018, mjini Dodoma.
Waziri
wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Prof. Joyce Ndalichako (Mb),
akimpongeza kwa furaha na bashasha Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt.
Philip Isdor Mpango (Mb), kwa kufanikisha kuandaa na hatimaye kupitishwa
kwa Bajeti Kuu ya Serikali ya kihistoria ya shilingi trilioni 31.7 ya
Mwaka wa Fedha 2017/2018, mjini Dodoma.
Waziri
wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kushoto),
akiteta jambo na maafisa waandamizi wa Wizara yake nje ya ukumbi wa
Bunge mjini Dodoma, baada ya Bunge kupitisha kwa kishindo Bajeti Kuu ya
Serikali ya shilingi trilioni 31.7.
Waziri
wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), akipongezwa na
Askari wastaafu wa Jeshi la KAR waliopigana Vita Kuu ya Pili ya Dunia
mwaka 1939-1945 baada ya Bunge kupitisha kwa kishindo Bajeti Kuu ya
Serikali ya shilingi trilioni 31.7, bungeni mjini Dodoma.
Waziri
wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) na Naibu wake
Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi
waandamizi wa Wizara hiyo baada ya Bunge kupitisha Bajeti Kuu ya
Serikali ya Shilingi trilioni 31.7 mjini Dodoma.
Waziri
wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) akimshukuru na
kumpongeza Naibu wake Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), kwa ushirikiano mkubwa
aliompatia hadi kufanikisha kazi kubwa ya kuandaa na kusimamia Bajeti
Kuu ya Serikali ya shilingi trilioni 31.7 iliyopitishwa na Bunge kwa
kishindo mjini Dodoma.
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Wizara ya Fedha na
Mipango).
Post a Comment