Mfanyabiashara mkubwa nchini, Mohammed Dewji ambaye alikuwa na mpango wa
kutaka kuinunua klabu ya Simba pia kuisaidia klabu hiyo katika mambo
mbalimbali ameonyesha kusikitishwa na viongozi wa klabu hiyo kusaini
mkataba bila kumshirikisha.
Klabu ya Simba imeingia mkataba wa miaka mitano na kampuni SportPesa ya udhamini wenye thamani ya 4.9 Bilioni
"Inasikitisha kuwa uongozi wa Klabu ya Simba umesaini mkataba wa
udhamini wa muda mrefu bila kunishirikisha. Kwa muda mrefu nimeweka
nguvu zangu kwenye klabu" alisema Mohammed Dewji kupitia ukurasa wake wa
Twitter
Post a Comment