Jopo la madaktari bingwa wa Shirika la Stemm la Marekani kwa
kushirikiana na Serikali, limeamua kuwapeleka Marekani kwa matibabu
majeruhi watatu wa ajali ya wanafunzi wa shule ya Lucky Vicent iliyoua
wanafunzi 32, walimu wawili na dereva.
Majeruhi hao ambao wamelazwa katika hospitali ya mkoa ya Mount Meru ni
Jofrey Tarimo, Doreen Mshana na Sadia Awadh wanatarajiwa kusafirishwa
kwenda Marekani wakiambatana na wazazi wao, daktari na muuguzi wa
hospitali ya mkoa wa Arusha.
Matibabu hayo yatatolewa kwa ufadhili wa madaktari hao kutoka Marekani
ambao walikuwa miongoni mwa watu wa kwanza kuwasidia wanafunzi hao
kutoka kwenye gari lililo pata ajali, wakiwa njiani kuelekea Ngorongoro
na Serengeti kutalii.
Daktari mkuu wa hospitali Mount Meru, Wonanji Thimos amesema kuwa
Serikali kwa kushirikiana na madaktari hao imeshaanza taratibu za
kuwasafirisha majeruhi hao kwa ajili ya matibabu zaidi.
Dk Thimos amesema taratibu za safari zikikamilika majeruhi hao watasafirishwa kwenda Marekani wakati wowote kuanzia sasa.
Post a Comment