Miaka
tisa baada ya kuvuliwa upadri wa Kanisa Katoliki, Privatus Kargendo
jana alifunga ndoa na mchumba wake Rose Birusya. Ndoa hiyo ilifungwa
katika Kanisa la Mtakatifu Petro jijini Dar es Salaam katika misa
iliyoongozwa na Padri Stefano Kaombe.
Kabla
ya kuvuliwa upadri, Karugendo alikuwa Padri wa Jimbo la Rulenge-Ngara
kabla ya Papa Benedict XVI kumvua daraja hilo kwa madai ya kukiuka
maadili ya kanisa katoliki.
Septemba
14, mwaka 2008 Karugendo alitangazwa kuwa ni muumini mlei asiye na
daraja la upadri tena kupitia hati ya Papa yenye namba Protokali
4182/08.
Ingawa
sababu za kuvuliwa kwake hazikuwekwa wazi kwa jamii zaidi ya kusema
amekiuka kanuni za kanisa hilo, watu wengi walihusisha tukio hilo dhidi
ya andiko lake kuhusu UKIMWI na matumizi ya mipira ya kiume (condoms).
Baada
ya kuvuliwa cheo hicho, Karugendo sasa ni mchambuzi wa masuala ya
kisiasa na kijamii katika vyombo mbalimbali vya habari ikiwemo gazeti la
Mwananchi.
Waumini
waliokuwamo katika misa ya ndoa hiyo, walimpongeza Karugendo na kusema
kuwa uamuzi wake wa kufunga ndoa katika Kanisa Katoliki umeonyesha kuwa
hana tatizo nalo licha ya kuvuliwa cheo hicho.
Mapadri
wa Kanisa Katoliki hawaruhusi kuoa ikiaminika ili waweze kujikita zaidi
katika kushughulikia masuala ya kanisa bila kuwa na kitu cha kuwaondoa
humo ikiwa ni pamoja na familia.
Post a Comment