Mahakama
ya Hakimu Mkazi Kisutu imetoa hati ya kumkamata msanii, Agnes Gerald
maarufu kama Masogange kwa kushindwa kuhudhuria kwenye kesi ya kutumia
dawa za kulevya inayomkabili.
Hati hiyo ilitolewa jana mbele ya Hakimu Mkazi mkuu, Wilbroad Mashauri, wakati kesi hiyo ilipotajwa.
Wakili
wa Serikali, Adolf Mkini alidai mahakamani hapo kwamba upelelezi wa
kesi hiyo upo hatua za mwisho, lakini mshtakiwa, wadhamini wake na
wakili wake hawakufika hivyo wakili Nkini akaomba mahakama itoe hati ya
kumkamata mshtakiwa huyo kwa sababu ni mara ya pili ameshindwa kufika
mahakamani hapo.
Hakimu Mashauri alikubali maombi ya wakili wa Serikali na kutoa hati ya kumkamata mshtakiwa ambaye ni Masogange.
Msanii huyo aliwahi kuonywa akitakiwa aheshimu mahakama kutokana na kutokuwapo kwenye kesi yake ilipotajwa.
Katika
kesi hiyo namba 77 ya mwaka 2017, Masogange anadaiwa kuwa kati ya
Februari 7 na 14 mwaka huu, katika maeneo yasiyojulikana ndani ya jiji
la Dar es Salaam, alitumia dawa za kulevya aina ya heroin(Diacety
Imophine). Pia inadaiwa kati ya Februari 7 na 14, 2017 alitumia dawa za
kulevya aina ya oxazepam.
Post a Comment