Mbunge
wa Kibamba, John Mnyika jana alibeza majibu ya Serikali kuhusu maji
yanayotoka katika Bomba la Ruvu Juu, akisema mradi huo haujaanza kufanya
kazi badala yake Serikali inatoa majibu yasiyo na uhalisia.
Katika
swali la nyongeza, mbunge huyo alisema majibu ya Serikali kuhusu mradi
huo kuwa umeanza kusambaza maji katika maeneo ya Mlandizi na vitongoji
vyake; Visiga, Misugusugu, Soga, Korogwe, Picha ya Ndege, Kwa Mathias na
maeneo mengine hayana ukweli.
Katika
swali la msingi, Mbunge wa Viti Maalumu (Chadema), Mary Deo Muro
alitaka kujua ni lini Serikali itawasambazia maji wananchi waishio
pembezoni mwa Bomba la Ruvu Juu, Mlandizi hadi Dar es Salaam hasa maeneo
ya Pangani, Lumumbana, Kidumu na Zogowale.
Naibu
Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Isack Kamwelwe alisema kwa sasa maeneo
mengi yameanza kupata maji ya kutosha ndani ya kilomita 12 pembezoni mwa
Bomba Kuu la Ruvu Juu na kwamba, baadhi ya maeneo ambayo hayajaanza
kupata maji, huduma hiyo itapatikana baada ya miradi mipya.
“Kwa
kuanzia, mkandarasi M/S Jain Irrigation System Limited ameanza kazi ya
ujenzi wa mabomba ya usambazaji maeneo ya Malamba Mawili, Msigani, Mbezi
Luis, Msakuzi, Kibamba, Kiluvya, Mlonganzila na Maili Moja na
atakamilisha kazi hiyo mwaka huu,” alisema Kamwelwe.
Post a Comment