Gari
Maalumu la kurusha matangazo ya moja kwa moja la kituo cha Luninga cha
Clouds likiwa katika eneo la Serengeti kwa ajili ya kurusha matangao ya
moja kwa moja ya kipindi cha Clouds 360.
Watangazaji
wa Kipindi cha Clouds 360 ,Sam Sasali na James Tupatupa wakifungua
kipindi katika eneo ambalo ni makazi ya Viboko ndani ya Hifadhi ya Taifa
ya Ngorongoro.
Watangazaji
wa Clouds 360 ,Sam Sasali na James Tupatupa wakiongea na Meneja
Mawasilino wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Pascal Shelutete
akizungumza jambo na watangazaji hao wakati wakifanya mahojiano.
Mkurugenzi wa Utalii na Masoko wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Ibrahim Musa akizungumza jambo na Mtangazaji Sam Sasali.
Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti William Mwakilema akizungumzia sifa za hifadhi hiyo ya pili kwa ukubwa .
Mwekezaji
katika Sekta ya Utalii,Wily Chamburo (wa pili toka kulia) akifurahia
jambo na Mkurugenzi wa Utalii na Masoko wa TANAPA,Ibrahim Musa (aliyevaa
koti) pamoja na Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti ,Wiliam
Mwakilema (kushoto) na Meneja Mawasiliano wa TANAPA ,Pascal
Shelutete.(kulia).
Watangazaji
Baby Kabaye na Hassan Noma wakifanya mahojiano na Mwekezaji katika
Sekta ya Utalii,Wily Chamburo wakati kipind cha Couds 360 kiliporushwa
moja kwa moja kutoka Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.
Watangazaji
Baby Kabaye na Hasan Ngoma wakifanya mahojiano na Mkurugenzi wa Utalii
na Masoko wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Ibrahim Musa wakati
kipindi cha Clouds 360 kiliporushwa moja kwa moja kutoka Hifadhi ya
Taifa ya Serengeti.
Mtangazaji
wa Sport 360 katika kipindi cha Clouds 360 ,James Tupatupa akifanya
mahojiano na Meneja Mawasiliano wa TANAPA,Pascal Shelutete wakati
akizungumzia Utalii wa kimichezo pamoja na namna TANAPA inavyoshiriki
katika kukuza Michezo mbalimbali nchini.
Naibu
Waziri wa Maliasili na Utalii,Mhandisi Ramo Makani akitoa neno la
Shukrani wakati kipindi cha Clouds 360 kilipokuwa kikihitimisha ziara
yake katika Hifadhi ya Taifa za Serengeti.
Wadau
waliokuwepo katika shughuli nzima ya urushwaji wa kipindi cha Clouds
360 wakifuatilia kwa karibu matukio yaliyokuwa yakiendelea.
Watangazaji
wa Kipindi cha Clouds 360 wakiwa katika picha ya pamoja na Wadau mara
baada ya kuhitimisha ziara ya urushwaji wa kipindi hicho katika Hifadhi
ya Taifa ya Serengeti.
Post a Comment