PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: TANZANITE ONE YATOA MILIONI 15 KWA SACCOS YA WANAWAKE SIMANJIRO ILI KUWAKWAMUA KIUCHUMI
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
Mkurugenzi mwenza wa kampuni ya  Tanzanite one Faisal Juma akimkabidhi  msaada wa shilingi milioni 15 kiongozi wa saccos ya wanawa...




Mkurugenzi mwenza wa kampuni ya  Tanzanite one Faisal Juma akimkabidhi  msaada wa shilingi milioni 15 kiongozi wa saccos ya wanawake wafugaji wa kata ya Naisinyai mapema jana ili wajikite katika ufanyaji wa biashara mbali na kutegemea ufugaji tu

NA: ANDREA NGOBOLE PMT

Wananchi wa jamii ya wafugaji wanaoishi katika kata ya Naisinyai wilaya ya Simanjiro inayopakana na machimbo ya Tanzanite wameshauriwa kuanza kujikita katika ujasiriamali badala ya kutegemea mifugo pekee.

Mkurugenzi mwenza wa kampuni Tanzanite One,Faisal Juma alitoa wito huo jana wakati akitoa msaada wa sh 15 million kwa wanawake wa Kata hiyo ili kuanzisha chama cha kuweka na kukopa(SACCOs).

Juma alisema, wananchi wa Naisinyai wamepata fursa ya kuwa katika eneo ambalo yanachimbwa madini ya Tanzanite  hivyo ni muhimu  wanufaike nayo kwa kujiunga katika vikundi vya ujasiriamali na kufanyabiashara ,kuchimba na kuuza  madini hayo.

"Sisi kama Tanzanite One tunawajibu kuwasaidia kuwa wajasiriamali kwani tunachimba madini katika kata yenu na huu ni msaada kwa wajasiriamali lakini bado tutaendelea kusomesha watoto wa Kaya masikini na kutoa Michango mingine"alisema

Alisema mabadiliko ya tabia nchi yameathiri sana mifugo hivyo ili kutoathiri maisha ya wafugaji wanapaswa kuwa na mbadala wa kidogo wa kuwasaidia kimaisha.

Awali mwenyekiti wa kijiji cha Naisinyai,Taiko Laizer alishukuru michango wawekezaji na kuwataka kupanua wigo wa kutoa ajira kwa wananchi wa Naisinyai hasa wanawake.

'Tunajua mmewapa ajira vijana wa hapa lakini tunaomba zinapotokea ajira hasa wanawake tuongezewe"alisema

Naye Diwani wa viti maalum Kata ya Naisinyai Paulina Masekeni aliahidi fedha waliopatiwa
Wanawake wa kata hiyo zitatumika kuanzisha vikundi vya ujasiriamali kama walivyo omba.



About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top