Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe
(kushoto) akipokelewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sanaa na
Utamaduni Bagamoyo (TaSUBA), Dkt. Herbet wakati alipowasili katika
taasisi hiyo kuzindua vitendea kazi 4 Aprili, 2017 Wilayani Bagamoyo
Mkoani Pwani.
Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe
(mwenye tai nyekundu) akiwa ameongozana na Mkurugenzi Mtendaji wa
Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBA) Dkt. Herbet Makoye
pamoja na viongozi wengine na watendaji wa TaSUBA wakati alipowasili
katika taasisi hiyo kuzindua vitendea kazi 4 Aprili, 2017 Wilayani
Bagamoyo Mkoani Pwani.
Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe
akiwa ameongozana na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sanaa na
Utamaduni Bagamoyo (TaSUBA), Dkt. Herbet Makoye pamoja na watendaji
mbalimbali wa Wizara na wa taasisi hiyo kuelekea kuangalia maeneo
mbalimbali ya taasisi 4 Aprili, 2017 Wilayani Bagamoyo Mkoani Pwani.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBA), Dkt.
Herbet Makoye akimuonyesha Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na
Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe jinsi maji ya bahari yalivyoharibu
kingo za taasisi hiyo wakati alipowasili katika taasisi hiyo kuzindua
vitendea kazi 4 Aprili, 2017 Wilayani Bagamoyo Mkoani Pwani.
Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe
akionyeshwa baadhi ya vifaa vilivyomo ndani ya Studio za Taasisi ya
Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBA) wakati alipowasili katika taasisi
hiyo kuzindua vitendea kazi 4 Aprili, 2017 Wilayani Bagamoyo Mkoani
Pwani.
Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe
akipiga nyimbo kwa kutumia kinanda ndani ya moja ya Studio za Taasisi ya
Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBA) wakati alipowasili katika taasisi
hiyo kuzindua vitendea kazi 4 Aprili, 2017 Wilayani Bagamoyo Mkoani
Pwani.
Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe
akiongea na wafanyakazi wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo
(TaSUBA), wageni waalikwa pamoja na wanafunzi wa taasisi hiyo kabla ya
uzinduzi wa vitendea kazi vya taasisi hiyo 4 Aprili, 2017 Wilayani
Bagamoyo Mkoani Pwani.
Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe
akizindua rasmi vifaa vya Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo
(TaSUBA), 4 Aprili, 2017 Wilayani Bagamoyo Mkoani Pwani.
Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe
akipokea zawadi za picha za kuchora toka kwa Mkurugenzi wa Taasisi ya
Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBA), Dkt. Herbet Makoye wakati
alipowasili katika taasisi hiyo kuzindua vitendea kazi vya taasisi hiyo 4
Aprili, 2017 Wilayani Bagamoyo Mkoani Pwani.
Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe
(mwenye tai nyekundu) akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa
Taasisi ya Sanaa na Utamaduni (TaSUBA) pamoja na watendaji wengine wa
Wizara mara baada ya kuzindua vitendea kazi vya taasisi hiyo 4 Aprili,
2017 Wilayani Bagamoyo Mkoani Pwani.
Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe
(mwenye tai nyekundu) akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa
Taasisi ya Sanaa na Utamaduni (TaSUBA), Watendaji waWizara pamoja na
wageni toka nje ya nchi mara baada ya kuzindua vitendea kazi vya taasisi
hiyo 4 Aprili, 2017 Wilayani Bagamoyo Mkoani Pwani.
(PICHA ZOTE NA BENEDICT LIWENGA-WHUSM)
Na Lorietha Laurence.
Waziri
wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe amezindua
Vifaa vya kufundishia vyenye thamani ya shilling 100 kwa ajili ya
Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo(TaSUBa) vitavyowawezesha
wanafunzi kujifunza kwa vitendo namna ya kutengeneza picha jongefu.
Akizungumza
wakati wa uzinduzi huo leo Wilayani Bagamoyo, Dkt.Mwakyembe amesema
kuwa vifaa hivyo ni muhimu katika maendeleo ya kitaaluma ya wanafunzi wa
Taasisi hiyo katika kuwaongezea ujuzi katika vitendo na baadaye kuwa
watendaji bora na makini.
“Vifaa
hivi ni tija katika kuhakikisha kuwa wanafunzi wanajifunza kwa vitendo
na hivyo kuzalisha watu wenye taaluma zenye tija na zenya kuleta matokeo
chanya kwa ajili ya maendeleo nchi”alisema Mhe.Dkt.Mwakyembe.
Aliongeza
kwa kuhaidi kuwa atahakikisha viongozi mbalimbali wakiwemo Mawaziri na
Mabalozi wanapata fursa ya kuitembelea TaSUBa ili wajionee kwa macho
hazina kubwa waliyonayo katika kukuza na kuendeleza sanaa na utamaduni.
Aidha
aliupongeza viongozi na walimu wa TaSUBa kwa jitihada wanazozifanya za
kutoa elimu kwa vijana jambo ambalo linawajengea uwezo wa kujiajiri
kupitia taaluma ya sanaa hivyo kuondoa utegemezi na kukuza uchumi wa
nchi.
Naye
Katibu Tawala wa Wilaya ya Bagamoyo Bibi Erica Yegela kwa niaba ya Mkuu
wa Wilaya hiyo alisema Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo(TaSUBa)
ipo kwa ajili ya maslahi ya Watanzania wote na hivyo wanakaribishwa
kujiunga na kujifunza sanaa,utamaduni na uandaaji wa vipindi.
Kwa
Upande wake Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo
(TaSUBa) Dkt. Herbert Makoye ameishukuru Serikali kwa kutoa fedha za
maendeleo kiasi cha shilling millioni 100 amabazo zimefanikisha kununua
vifaa vya kufundishia kwa vitendo.
“Tunaishukuru
Serikali kwa kutupatia kiasi hiki cha fedha ambapo kwa kiasi kikubwa
kimefanikisha manunuzi ya vifaa hivi vya kufundishia na huu ni mwanzo
mzuri nasi tunaahidi kutumia ipasavyo katika kuzalisha wanataaluma
hodari” alisema Dkt. Makoye.
Aliongeza
kwa kusema kuwa licha ya kufanikiwa katika kununua vifaa kumekuwapo na
changamoto mbalimbali zinazoikabili- Taasisi hiyo ikiwemo upungufu wa
wafanyakazi huku wengi wao wakiwa wamestaafu,uhaba wa ofisi za waalimu
na wafanyakazi pamoja na miundo mbinu chakavu.
Post a Comment