Wananchi
wa jamii ya wafugaji katika kijiji cha Mbukkeni ,kata ya Harashi wakiwa
wamezuia msafara wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Ardhi,Maliasili na
Utalii iliyofanya ziara kutembelea Pori tengefu la Loliondo kupata hali
halisi ya mgogoro uliopo .
Magari
yaliyokuwa yamebeba wajumbe wa kamati hiyo yakiwa yameegeshwa baada ya
wananchi kuzuia msafara huo wakishikiza kamati kusikiliza kero
walizokuwa nazo.
Wajumbe wa kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi,Maliasili na Utalii walilazimika kushuka na kuzungumza na wananchi hao.
Wajumbe wa kamati hiyo wa kizungumza na wananchi wa jamii ya wafugaji katika eneo hilo.
Vijana wa jamii ya wafugaji wakiwa wamebeba silaha za jadi .
Mbunge
wa Jimbo la Siha ambaye pia ni mjumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya
Ardhi,Maliasili na Utalii,Godwin Mollel akizungumza na wananchi wa jamii
ya Wafugaji katika kijiji cha Mbukeni baada ya kuzuia msafara wa kamati
hiyo.
Wananchi
wa jamii ya wafugaji katika kijiji cha Mbukeni,Kata ya Harashi ,tarafa
ya Loliondo wilayani Ngorongoro wamezuia kwa muda msafara wa kamati
ya kudumu ya Ardhi,Maliasili na Utalii wakishinikiza kusikilizwa kero
zao.
Katika
Pori tengefu la Loliondo lililopo wilayani Ngorongoro mkoani Arusha
kumekuwa na mgogoro uliodumu kwa zaidi ya miaka 25 sasa huku suluhu ya
utatuzi wa kiini cha mgogoro huo kikitafutiwa ufumbuzi.
Kamati
ya kudumu ya Bunge ya Ardhi,Maliasili na Utalii imetembelea maeneo
mbalimbali ya Pori hilo kwa lengo la kujionea hali halisi kabla ya kutoa
tamko juu ya mgogoro huo ambapo ikiwa njiani kuelekea Mamlaka ya
Ngorongoro ikakutana na kundi la wafugaji wakiwa wamezuia barabara
Hatua
ya wafugaji hao kusimamisha msafara wa kamati inakuja muda mfupi baada
ya kamati kufanya kikao na wawakilishi wa wafugaji hao,kikao
kilichofanyika katika ukumbi wa Hotel ya Domel uliopo waso loliondo.
Wajumbe
wa kamati ya Ardhi,Maliasili na Utalii waliozungumza
,Sebastian Kapufi na Dkt Godwin Mollel wamesema hatua ya wafugaji hao
kuzuia msafara wa kamati ililenga kuvuruga ziara hiyo.
Wajumbe
wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Ardhi ,Maliasili na Utalii wakiwemo
wataalamu na wanasheria imewasili Loliondo ikiongozwa na Mwenyekiti wake
Mhandisi,Atashasta Nditiye na kufanya ziara ya kutembelea eneo lenye
ukubwa kilomita 1500 za mraba linalokusudiwa kurejeshwa katika hifadhi .
Post a Comment