wajumbe wa kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi,Maliasili na Mazingiraa wakiwa wanapata maelezo juu ya mchanaga unaohama yaani shifting sand toka kwa mtaalamu Walter Mairo hayupo pichani |
Akizungumza
mbele ya kamati hiyo, akiwa na wananchi wenye mabango,Mwenyekiti wa kijiji
Mbuken, Parmitoro Mbotoony alisema
wanapinga mpango wa kumegwa ardhi hiyo kwani ndio tegemeo la maisha yao ya kila siku.
Hata hivyo,
wajumbe wa kamati hiyo,Richard Ndasa bunge wa jimbo la Sumve na mbunge wa jimbo
la Siha,Dk Godfrey Mollel na mbunge jimbo la Babati mjini, Paulina Gekul
waliwasihi wananchi hao, kuwa watulivu kwani maoni yao yamechukuliwa.
Akizungumza
na wananchi hao,Dk Mollel aliwataka kuwa watulivu kwani,kamati hiyo haikufika
Loliondo kuchukuwa ardhi ya vijiji na itahakikisha maslahi ya wananchi wa
Loliondo yanalindwa .
Akizungumza
na waandishi wa habari baada ya tukio hilo, Mwenyekiti wa kamati hiyo, Mhandisi Atashasta
Nditiye alieleza kusikitishwa na kitendo cha viongozi wa wafugaji kwahadaa wananchi na kuwaandaa ili kuifanyia
vurugu kamati yake.
Nditiye
alisema nia ya ziara yao ya loliondo, haikuwa kufanya mikutano ya hadhara bali
ni kulipitia eneo lenye mgogoro ili kujifunza na baadaye kutoa ushauri kwa
serikali kwa maslahi mapana ya Taifa.
Hata hivyo,
alisema walikutana na wawakilishi wa wananchi, wawakilishi wa mashirika yasiyo
ya kiserikali (NGOs) na Mkuu wa wilaya ya Ngorongoro,Rashid Taka na kupokea
maoni yao.
“tumewajua
waliwapeleka wananchi kufunga barabara na kutaka kutufanyia vurugu na hasa
baada ya kuwapotosha wananchi, sisi hatujaja kwa nia mbaya”alisema
Waziri wa Maliasili
na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe, akizungumzia mgogoro huo, alikanusha
taarifa kuwa wizara yake imeiteka kamati na kueleza kamati ipo huru inatimiza
wajibu wake.
“hii kamati
imekuja kuangalia maeneo ya hifadhi hasa
kutokana na umuhimu wake kwani eneo hilo la ikolojia ya Serengeti linaingizia
serikali dola milioni 200 kila mwaka”alisema
Mbunge wa
jimbo la Mpanda mjini, Sebastian Kapufi, aliomba kamati hiyo ya bunge kuachwa
huru ili itemize kazi yake ya kuishauri serikali kwa maslahi ya taifa.
Kwa zaidi ya
miaka 20 kumekuwepo mgogoro wa ardhi,katika eneo la pori tengefu la Loliondo na
safari hii mgogoro umelipuka kutokana na uamuzi wa wizara ya maliasili kutaka
kutenga eneo la kilomita za mraba 1500 ndani ya eneo la kilomita 4000 za pori
tengefu ili lihifadhiwe.
Eneo hilo
linaelezwa kuwa ndilo lina vyanzo vya maji na ni mazalia ya wanyamapori katika
eneo la ikolojia ya Serengeti.
Post a Comment