Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba jana alikuwa katika wakati
mgumu kueleza sababu za kuonekana mara kwa mara katika shughuli za
kiserikali kuliko zile zinazohusu vyama vya upinzani.
Profesa Lipumba ambaye ana mgogoro na chama chake, alikuwa katika
kipindi cha Funguka kinachorushwa na kituo cha televisheni cha Azam TV
akiwa na mtangazaji mkongwe, Tido Mhando.
Akijibu swali hilo, Profesa Lipumba, ambaye licha ya kuvuliwa uenyekiti
wake bado anatambuliwa na Msajili wa Vyama vya Siasa, alisema kuonekana
kwake kwenye shughuli hizo kusichukuliwe kuwa yuko karibu na Serikali,
bali huo ni utamaduni aliojiwekea muda mrefu.
Profesa Lipumba alisema hawezi kukataa kuhudhuria shughuli za Serikali
kwa kuwa anatoka chama cha upinzani, sababu maendeleo hayana chama.
“Kama nimealikwa katika shughuli ambayo Rais anafungua miundombinu yenye
manufaa kwa Taifa zima, siwezi kuacha kwenda. Nitahudhuria, nitakwenda
tu kwa sababu maendeleo hayana chama.
“Sijaanza juzi kuhudhuria shughuli za kiserikali. Ukifuatilia utagundua
kuwa huo ni utamaduni wangu tangu zamani. Nikialikwa katika shughuli za
kiserikali na nikiwa na nafasi nimekuwa nikihudhuria,” alisema
Post a Comment