Wataalamu wa afya wameeleza kuwa kati ya asilimia 17 - 20 ya vifo vya wajawazito nchini husababishwa na kifafa cha mimba.
Daktari
wa Afya ya Jamii, Isack Maro amesema kifafa cha mimba ni miongoni mwa
magonjwa yanayowapata wajawazito na kusababisha vifo vingi katika nchi
zilizo Kusini mwa Jangwa la Sahara ikiwamo Tanzania.
“Hali
hii ambayo kitaalamu hujulikana kama pre-eclampsia, huonekana zaidi
wakati wa ujauzito wa kwanza, lakini inaweza kujirudia hata katika
ujauzito wa pili.
“Mjamzito
huwa na viashiria vitatu ikiwamo uwapo wa shinikizo la juu la damu,
kiwango kikubwa cha protini mwilini pamoja na kuvimba miguu au mwili.
Vitu hivi ndivyo hutoa bainisho sahihi la kitabibu,” amesema.
Download Application ya Udaku Special Blog Kwa Kubonyeza Hapa
Post a Comment