Aliyekuwa staa mkubwa wa muziki
wa Taarab Bongo, Mzee Yusuf ambaye kwa sasa amemrudia Mungu wake na kuwa
alhaji, amefunguka kuwa bado watu hawaamini kama kweli ameachana na
muziki wa kidunia hivyo wamekuwa wakimwalika kwenye misikiti mbalimbali
ndani ya Dar na mikoani hivyo kuwa mhadhiri wa kitaifa (kwa mujibu wa
Kamusi Sanifu, mhadhiri ni mtu anayetoa mhadhara, au mwalimu katika chuo
cha elimu ya juu hususan chuo kikuu).
Akizungumza baada
ya kuulizwa juu ya taarifa kwamba anafanya ziara kwenye misikiti
mbalimbali na kutoa mawaidha (kufanya mihadhara) ya kumtangaza Mungu kwa
nguvu zote, Mzee Yusuf alifunguka kuwa siyo kweli kwamba amepanga ziara
ya misikitini bali huwa anaalikwa kwa ajili ya kutoa mawaidha ya
Kiislamu.
“Siyo kwamba nimepanga ziara bali kila
ninapoingia kwenye misikiti mbalimbali kuswali, watu wamekuwa wakinitaka
nitoe neno kwa waumini hivyo nasimama, natoa mawaidha maana ndiyo
upande niliochagua kwa sasa wa kumtumikia Mungu wangu.
“Nimekuwa nikipata mialiko kutoka kwa
mashehe mbalimbali wa mikoani, ninakwenda kutoa neno maana watu wengi
hawaamini kama kweli nimeachana na muziki hivyo ninasafiri sana na
nikifika huko ndiyo wengine wanaamini na kuthibitisha.
“Kwa sasa nimeamua kusoma dini kiundani
ili nijue nini Mungu anataka na nini hataki, siyo kusoma Quran bali
nasoma dini niijue vizuri ,” alisema Mzee Yusuf, hata hivyo, watu
mbalimbali wanasema familia yake iko mguu sawa kujiandaa kufuata nyayo
zake.
Mwaka jana, Mzee Yusuf alitangaza
kuachana na muziki wa taarab kisha akaenda kuhiji Macca, jambo liliibua
mshtuko wa mashabiki wake lukuki wa bendi yake ya Jahazi.
Post a Comment