Mabingwa watetezi wa
Ligi Kuu Bara, Yanga ni baba lao hapa nchini, ni baada ya kuzizidi Simba
na Azam FC kwenye orodha ya Klabu Bora Afrika.
Hiyo ni kwa mujibu wa orodha iliyotolewa juzi Jumapili na mtandao mkubwa wa kimataifa wa FootballDatabase.
Kwa mujibu wa orodha
hiyo, Yanga inaongoza ubora Tanzania baada ya kujikusanyia pointi 1252
ikipanda kwa nafasi 14 huku ikikamata nafasi ya 332 barani Afrika.
Azam waliochukua
Kombe la Mapinduzi hivi karibuni, wenyewe wanashika nafasi ya pili
nchini Tanzania kwa pointi zao 1249 na kukamata nafasi ya 353 barani
Afrika.
Simba wanafunga orodha ya Tanzania katika nafasi ya tatu kwa pointi zao 1247 katika nafasi ya 358 barani Afrika.
Katika orodha hiyo, Simba ndiyo timu iliyoimarika zaidi kwa kupanda kwa nafasi 38 toka nafasi waliyokuwa mwaka jana.
Mabingwa wa
kihistoria Al Ahly wanaendelea kuongoza barani Afrika wakifuatiwa na
Esperance de Tunisia, TP Mazembe, AS Vita na Etoile du Sahel
wakikamilisha tano bora.
Yanga, inatarajiwa
kuiwakilisha nchi katika Ligi ya Mabingwa Afrika huku Azam ikicheza
Kombe la Shirikisho Afrika, Simba wameporomoka kwa kuwa ni muda mrefu
sasa hawajashiriki michuano ya kimataifa.
Post a Comment