PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: TAZAMA KIKI ZA MAPENZI ZINAVYOWAPELEKA WASANII WA BONGOFLEVA
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
BAADA ya misukosuko ya kupanda na kushuka kwa matukio mengi, tayari mchakamchaka wa 2017 umeanza, katika burudani ya kiz...

BAADA ya misukosuko ya kupanda na kushuka kwa matukio mengi, tayari mchakamchaka wa 2017 umeanza, katika burudani ya kizazi kipya mwishoni mwa mwaka uliopita msanii Darassa ndiye alikuwa habari ya mjini.

Miezi 12 iliyopita tulishuhudia matukio mengi ya kujiongezea umaarufu ‘kiki’ ya aina tofauti huku yale ya watu maarufu hasa wasanii kuandikwa na kuzungumzwa kwa wingi kutokana na maisha yao ya kimapenzi nayo yalipata nafasi kubwa.
Ukiachana na Diamond na Zari ambao uhusiano wao ulikuwa gumzo kama ilivyokuwa kwa mastaa kadhaa wakiwemo Jux na Vanessa Mdee, msanii wa Bongo Fleva, Zuwena Mohamed ‘Shilole au Shishi Baby’naye hakuwa nyuma katika upande huo.
shilole-12Shilole akiwa na mpenzi wake wa sasa Boy Caro.
Shilole, 28, ambaye alianza kutamba katika maigizo kabla ya baadaye kuegemea zaidi katika muziki, ni mama wa mabinti wawili, Joyce na Rahma.
Joyce ndiye wa kwanza na inaelezwa kuwa anaelekea kutimiza umri wa miaka 14, huku Rahma akitarajiwa kutimiza umri wa miaka 10 baadaye mwaka huu.
Pamoja na hali hiyo, ndani ya miaka mitatu iliyopita Shilole amekuwa akitajwa kuhusishwa kuwa katika uhusiano wa kimapenzi na wanaume kadhaa. shilole-14
Akiwaza jambo.
Licha ya mwenyewe kukiri kuwa aliwahi kuingiliwa kinguvu na mwanaume wakati akiwa na umri wa miaka 15, bado inaonyesha hajaamua kuondoa ‘jinamizi’ la mapenzi linalomuandama.
Mwaka 2013, uhusiano wake na aliyekuwa chipukizi wa Bongo Fleva, Ally Timbulo ulizungumzwa na wengi lakini baadaye wawili hao walivurugana kisha Timbulo akatua kwa staa wa Bongo Movie, Jacqueline Pentezel ‘Jack Chuzi’. Mahaba ya Timbulo na Shilole yalidumu kwa zaidi ya miezi sita.
Inadaiwa kuwa baada ya hapo Shilole alikabidhi moyo wake kwa Mbongo Fleva mwingine, Elias Barnaba ‘Barnaba Classic’, ambaye sasa naye ni baba wa mtoto mmoja aitwaye Steve aliyezaa na mwanamke mwingine aitwaye Zuu.
shilole-9
Shilole akijiachia na mpenzi wake.
 
Penzi la Shishi na Barnaba nalo halikuchukua muda mrefu, sababu haikujulikana lakini Barnaba akaamua kuelekeza nguvu kwa mchumba wake wa siku nyingi, mama Steve ambaye ndiye anayeishi naye mpaka sasa.
Kama filamu vile, Shilole akatulia kwa muda kisha akamkabidhi moyo wake Nurdin Mlawa a.k.a Nuh Mziwanda ambaye aliuchukua moyo huo na kuusafisha vizuri kisha akamfanya ‘mtoto’ kuwa mtu mwenye furaha kubwa. shilole-7
Wapenzi hao walionyeshana mahaba yao waziwazi, kuanzia kwenye mitandao, mitaani, kwenye shoo na hata sehemu nyingine nyingi walikuwa pamoja wakiongozana.
Ikadaiwa kuwa ubabe wa Shilole ukawa kikwazo kwa Nuh ambaye mara kadhaa aliwahi kupokea vibao vya hapa na pale hadharani kutoka kwa laazizi wake huyo, baada ya hadithi za wameachana-wamerudiana kutokea mara kadhaa, mwisho wake wakamwagana rasmi.
Wiki kadhaa baada ya penzi hilo kufa, tetesi zikaibuka kuwa Shishi Baby ameanguka mikononi mwa dogodogo mwingine, Nedy Music ambaye ni mwanamuziki wa Bongo Fleva.
Boti ya mapenzi ya wawili hao inadaiwa haikudumu hasa kwa kuwa haikupata kiki, muda mfupi baadaye Shilole kwa mara nyingine ikaelezwa kuwa kijana kutoka Tanzania House of Talent (THT), Hamadai kanasa kwenye penzi la mama wawili huyo.
Watu wa karibu wa wasanii hao wakafunguka kuwa utofauti wa tabia zao ndiyo uliofanya maisha yao ya kuwa penzini kuwa mafupi. shilole-13
Mwishoni mwa mwaka jana mpaka sasa, Shishi Baby amenasa kwenye mikono ya kijana anayeitwa Adam maarufu kwa jina la Boy Caro.
Wameonekana kuwa pamoja wakiongozana sehemu nyingi, wakipiga picha, wakifurahia maisha na wamewahi kuhojiwa kwenye kituo kimoja cha redio hivi karibuni ambapo wakaelezea jinsi wanavyopendana na mipango yao ya baadaye. Boy Caro siyo msanii ila ni mzoefu wa jiji na anafanya biashara.
shilole-4
Shishi amechagua maisha yake ya mapenzi yawe sehemu ya umaarufu wake na ndiyo maana kila anapohama kutoka kwa mmoja kwenda kwa mwingine inakuwa rahisi kujulikana na anaitumia kama sehemu ya kujiongezea kiki.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top