Mkali wa muziki wa singeli Bongo, Man Fong amemtaja msanii mwenzake wa
bongo fleva na bongo movie, Shilole a.k.a Shishi Trump kuhusika katika
ujenzi wa nyumba yake ambayo anataraji kuijenga wakati wowote kutoka
sasa.
Man Fongo aliyekuwa katika mahojiano
kwenye kipindi cha Ujenzi cha EATV, amesema mtu pekee aliyemuhamasisha
kujenga nyumba ni Shilole, na hiyo ni baada ya siku moja kutembeea
nyumbani kwa Shilole na kukuta vitu ambavyo yeye aliona ni vya ajabu na
kujikuta anavipenda na kutamani kuwa navyo katika nyumba yake.
Alisema jambo la kwanza alilofanya
kukusanya fedha na kununu kiwanja ambacho kiko tayari na amekinunua
maeneo ya Kimara Bonyokwa na muda wowote ataanza kuporomosha mjengo
wake.
Amesema hawezi kumsahau Shilole kwa
kumpa hasira za kuweka mjengo huo, ambao amesema ataujenga taratibu kwa
kadri atakavyokuwa anapata pesa na anatamani uwe na vitu vyote vizuri
kama ambavyo huwa anaviona kwa washkaji zake hasa Shilole, licha ya kuwa
yeye ni mtoto wa uswahilin
"Sina nyumba, lakini nina kiwanja Kimara
Bonyokwa na Shilole ndiye aliyenipa hasira ya kumiliki mjengo wangu,
mimi ni mtu wa uswazi lakini kuna vitu ningependa kuviweka kwenye mjengo
wangu, natamani kuwa na vitu vizuri, kama ninavyoona kwa wenzangu.....
kwa mfano pale kwa Shishi nimeona amechora chora hivi kwa pembeni,
halafu juu kuna madude hivi mimi huwa naita ceiling board, nyie sijui
mnaitaje (Gypsum) eheee" Amesema Man Fongo.
Amewashauri vijana hususani wasanii
wenye uwezo na kipato kujenga nyumba zao, kwani ni muhimu na si lazima
kujenga haraka bali kwa utaratibu kadri watakavyokuwa wakipata pesa.
"Kama mimi ndo nimeanza kupata kipato
changu kidogo, nimeanza kununua kiwanja... kujenga hakuhitaji papara,
kama leo ukishindwa, zamu yako itakuja kesho" Alimalizia Man Fongo
Post a Comment