Title: BELLE 9 AWEKA WAZI SABABU ZA YEYE NA WASANII WENGINE KUIMBA NYIMBO NYINGI ZA MAPENZI
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5
Des:
Msanii wa Bongo Fleva, Belle 9 amefunguka sababu za yeye pamoja na wasanii wengi wa muziki huo kuimba nyimbo zenye ujumbe wa mapenzi...
Msanii
wa Bongo Fleva, Belle 9 amefunguka sababu za yeye pamoja na wasanii
wengi wa muziki huo kuimba nyimbo zenye ujumbe wa mapenzi zaidi ya
ujumbe mwingine
Belle
9 akijibu maswali ya mashabiki na wapenzi wa muziki kupitia Kikaangoni
ya EATV, amesema sababu kubwa ya yeye kutunga nyimbo za aina hiyo ni
biashara kwa kuwa ujumbe huo ndiyo unaopendwa zaidi na mashabiki wa
muziki.
Tunaimba
mapenzi kwa sababu za kibiashara, ukiimba mapenzi ndiyo watu wanakuwa
wepesi ku-catch tofauti na ukiimba vitu vingine, kwahiyo tunaimba
mapenzi kwa sababu za kibiashara kwa kuwa watu ndiyo wanapenda". Alisema
Belle 9.
Nyimbo nyingi ambazo ameimba Belle 9 na zika-'hit' zilikuwa na ujumbe wa mapenzi isipokuwa ule wa 'Nilipe Nisepe' ambao ulikuwa na ujumbe tofauti kabisa.
Baadhi
ya nyimbo hizo ni kama vile Sumu ya Penzi (uliomtoa), Masogange, Burger
Movie Selfie, Shauri Zao, Listen na ngoma yake mpya aliyoweka vionjo
vya Saida Karoli, Give it to me.
Akijibu
swali kuhusu mafanikio aliyoyapa hadi sasa katika muziki, Belle 9
alisema "Kuna mafanikio mengi nimeyapata, kubwa ikiwa ni kipato,
lakini nimeongeza watu, najitegemea, sitegemei tena mtu"
Post a Comment