Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi,
Charles Tizeba (kushoto), akizungumza na watafiti wa kilimo na
wanahabari (hawapo pichani), wakati alipotembelea shamba la jaribio la
mahindi yaliyoboreshwa kwa kutumia Teknolojia ya uhandisi jeni chini ya
mradi wa Wema katika Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Makutupora mjini
Dodoma leo. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Sayansi na
Teknolojia (COSTECH), Dk.Hassan Mshinda.
Mkurugenzi wa Utafiti na Maendeleo wa
Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi, Hussein Mansour akizungumza katika
mkutano huo kabla ya kumkaribisha Waziri Tizeba.
Mkutano ukiendelea.
Mshauri wa masuala ya Bioteknolojia Dk.Nicholaus Nyange (kulia), akitoa mada kuhusu, Bioteknolojia ya kisasa katika sekta
ya kilimo nchini.
Mshauri wa mradi wa Wema, Dk. Alois Kullaya (kulia), akitoa mada kuhusu utafiti wa mahindi yanayohimili ukame.
Taarifa ikitolewa mbele ya Waziri Tizeba (kushoto)
Safari ya kuelekea shamba la jaribio la mbegu za mahindi ikiendelea. Katikati ni Waziri Tizeba.
Mkurugenzi wa
Utafiti wa Kilimo Kanda ya Kati Makutupora, Leon Mroso (katikati),
akitoa ufafanuzi kuhusu shamba hilo la jaribio hilo.
Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi,
Charles Tizeba (kulia), akizungumza na watafiti wa kilimo wakati
alipotembelea jaribio la mahindi yaliyoboreshwa kwa kutumia Teknolojia
ya uhandisi jeni chini ya mradi wa Wema katika Kituo cha Utafiti wa
Kilimo cha Makutupora mjini Dodoma leo. Kushoto ni Mshauri wa mradi wa
Wema, Dk. Alois Kullaya na Mkurugenzi wa Utafiti wa Kilimo Kanda ya Kati
Makutupora, Leon Mroso.
Mshauri wa mradi wa Wema, Dk. Alois Kullaya (kushoto), akimuelekeza jambo Waziri Tizeba.
Taswira ya shamba hilo la jaribio la mbegu za mahindi lililopo Makutupora mkoani Dodoma.
Waziri Tizeba (wa sita kushoto), akiwa katika picha ya pamoja na watafiti wa kilimo baada ya kutembelea shamba hilo.
Dotto Mwaibale, Dodoma
SERIKALI imesema itaangalia upya
taratibu na kanuni zilizopo ili kuharakisha tafiti za kilimo
zinazofanyika nchini zianzekufanya kazi kwa wakati.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Kilimo
Mifugo na Uvuvi, Charles Tizeba wakati alipotembelea jaribio la mahindi
yaliyoboreshwa kwa kutumia Teknolojia ya uhandisi jeni chini ya mradi
wa Wema katika Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Makutupora mjini Dodoma
leo asubuhi.
"Binafsi nisema katika teknolojia hii ya
uhandisi jeni kwa hapa nchini tumechelewa kutokana na taratibu na
kanuni zetu kutuchelewesha kwani maarifa ya watafiti wetu hayawafii
walengwa kutokana na kanunu hizo" alisema Tizeba.
Alisema ni lazima serikali kuangalia
jambo hilo ili kufupisha matokeo ya utafiti wa wataalamu wetu kuendelea
kufanya hivyo ni kucheleweshana.
Alisema mbegu hii ambayo inafanyiwa
utafiti kwa wenzetu wa Afrika Kusini wameanza kuitumia wakulima wao
lakini kwa sisi kwa utaratibu wetu mbegu hiyo tutaanza kuitumia mwaka
2021 ni miaka minne zaidi.
"Tusisubiri taratibu hizi tutazungumza
na wenzetu wa Ofisi ya Mkamu wa Rais Mazingira na Tume ya Taifa Sayansi
na Teknlojia (Costech) ili kuona namna ya kupunguza taratibu na kanuni
hizo ambazo hazina tija kwa mkulima.
Alisema kama utafiti umefanyika na
ukatoa matokeo mazuri hakuna sababu ya kusubiri na kupoteza muda wa
matumizi ya teknolojia hiyo.
Alisema leo tabia nchi imeendelea kukua
na ukame lakini sisi tunajifunga katika jambo ili ni lazima tujipange na
kutumia teknolojia hii muhimu.
Akizugumzia kuhusu mtazamo hasi wa
baadhi ya wananchi kuhusu matumizi ya vyakula vya GMO alisema mitazamo
hiyo inachochewa na wanaharakati kwa faida zao binafsi na kama
wanaushahidi wa jambo hilo ni vizuri wakatoa ushahidi huo hadharani
badala ya kupotosha umma.
"Kama mtu anaushahidi huo namuomba
aniletee badala ya kuzungumza mitaani kwani wenzetu wa nchi zingine
wanatumia vyakula hivyo na kama vingekuwa si sahihi wangewezaji
kuvitumia" alihoji Tizeba.
Post a Comment