Serikali
imesema ipo tayari kushirikiana na wadau katika sekta ya habari
kubadilisha baadhi ya sheria na kanuni zinazoongoza tasnia ya habari
ambazo zinaonekana kubana na kukandamiza tasnia hiyo kwa kwendana na
mabadiliko ya wakati na teknolojia.
Waziri wa Habari,Sanaa
na Michezo, Nape Nnauye ametoa kauli yake wakati wa ziara yake
aliyoifanya katika vyombo vya habari vya IPP yenye lengo la kuangalia
changamoto ambayo sekta hii ambayo inakabiliana nazo. Waziri huyo
amesema wakati umefika sasa wa kubadilisha sheria na kanuni zinazobana
vyombo vya habari.
“Mimi kwa upande wangu
siamini kwamba kamati ya maudhui kazi yake ni kupiga faini, kazi yao
lazima itoke kwenye kupiga faini iende kwenye kuelezana. Sasa ukiwaambia
watakwambia sheria, kwahiyo sheria tukashughulike nayo basi na mimi
natamani kwakuwa mimi ndo ninayepeleka sheria bungeni, bahati nzuri
kanuni mwisho ni kwa waziri na ukisoma hukumu nyingi wanacheza na kanuni
so it’s me to change basi, na mimi huko ndo nataka twende,” alisema
Nape
“Lakini nikasema
nisiende kama ninavyohisi mimi niende kama mahitaji ya wadau yalivyo na
ndio maana ni swali hilo tu mna kikwazo wapi tukae chini tuone kama pana
uwezo wa kubadilisha tubadilishe.”
Kwa upande wake
Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dk
Hassan Abbas amevihakikishia vyombo vya habari nchini ushirikiano mzuri
katika kupata habari za serikali kutoka katika vitengo vyote vya
mawasiliano serikalini
“Niwahakikishieni ndugu
zangu wanahabari kuwa suala la upatikanaji wa habari kutoka serikali
litakuwa si la kusumbuana tena na tunatengeneza mfumo katika vitengo
vyote vya mawasiliano serikalini ili iwe rahisi kupata taarifa kutoka
kwetu,” amesitiza Dk Abass.
Post a Comment