Diamondakiwa amembeba mwanaye mchanga, Nillan.
|
Matarajio ya mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ ya
kumtumia mwanaye Nillan kupata mamilioni ya pesa kutoka kwa wadhamini
yanadaiwa kubuma kufuatia maelezo kuwa, baadhi ya makampuni yaliyokuwa
yamezungumza naye yameamua kujiweka pembeni kutokana na ukata wa pesa.
Awali, akizungumza
hivi karibuni, Diamond aliweka wazi kuwa, kabla hata mtoto hajazaliwa
kuna benki mbili ambazo zilimwaga dau la mamilioni ya pesa kwa ajili ya
kutumia picha ya mtoto huyo kwenye huduma zao lakini yeye alikuwa
hajaweka wazi ipi aingie nayo mkataba na kwa mkwanja upi.
Diamondakiwa amembeba mwanaye mchanga, Nillan.
Hata hivyo wakati mtoto huyo akikaribia
kufikisha mwezi mmoja, taarifa zilizotufikia zinadai kwamba baadhi ya
makampuni yaliyojitutumua kutaka kutoa mamilioni kwa ajili ya sura ya
mtoto huyo yameingia mitini.
Chanzo makini kilicho karibu na msanii
huyo kilidai kuwa, awali Diamond alikuwa amefanya mazungumzo na
makampuni na mabenki tofauti lakini kutokana na hali ngumu, baadhi
wamekaa kimya mpaka sasa.
“Kimsingi yale mamilioni ambayo Diamond
na Zari walitarajia kuyapata kutoka kwa makampuni na benki kama
ilivyokuwa kwa Tiffah, yamebuma. Mambo yamekuwa siyo.
“Inavyoonekana huku kubana pesa za dili
kwa Rais John Magufuli kumewafanya hata wale waliokuwa wakitaka kutoa
pesa ili wanunue sura ya Nillan wafanye uamuzi wa kupotezea.”
Zari (aliyelala) ikiwa ni saa chache baadea ya kujifungua
Umaarufu wa Nillan umechangia?
Aidha, wachambuzi wa mambo wameeleza
kuwa, kubuma kwa mapesa hayo kunaweza kuwa kumetokana na mtoto huyo
kutovuma kama ilivyokuwa Tiffah hivyo kuna ambao wameona kutoa pesa kwa
ajili ya sura yake ni sawa na kuzitupa.
“Kipindi cha Tiffah ilikuwa rahisi sana
benki na makampuni mbalimbali kutoa pesa ili kununua sura yake kwa kuwa
alikuwa ‘hot’ na pia fedha ilikuwa inapatikana kirahisi lakini ikimbukwe
huu ni utawala na Magu, pesa haitoki kirahisi.
“Pia Nillan mpaka sasa hawezi
kuishawishi benki yoyote itoe mamilioni kununua sura yake kwa kuwa hana
kiki kivile. Kwa mfano Tiffah alipozaliwa na kufunguliwa ukurasa wake wa
Insta, ndani ya siku mbili tu alikuwa na followers (wafuasi) 200,000
lakini kwa Nillan akiwa anakaribia kufikisha mwezi mmoja ana followers
69,000, hiyo inaonesha watu hawamshobokei na hata kibiashara sura yake
haiwezi kuwa kivile,” alisema Rashid Maguli wa Kinondoni ambaye ni
shabiki mkubwa wa Diamond.
Diamond na mpenzi wake, Zari
Hili linaweza kutokea pia
Ikazidi kudaiwa kuwa, kuna uwezekano kwa
mara ya kwanza Diamond akaamua kuionesha picha ya Nillan bila kuwa na
mdhamini au akapata wadhamini lakini akapewa ‘pesa mbuzi’ tofauti na
matarajio yake.
Diamond anasemaje?
Kufuatia kumwagika kwa ubuyu huo,
paparazi wetu alifanya jitihada za kumtafuta Diamond ambapo
alipopatikana alisema hawezi kulizungumzia suala hilo kwa kirefu kwa
kuwa bado mazungumzo yanaendelea na anaamini kila kitu kitaenda sawa.
“Kila kitu kinaenda sawa, niliongea na
baadhi ya wadhamini na kuwaambia wasubiri mtoto azaliwe, sasa amezaliwa
naamini kila kitu kitaenda sawa, hayo mambo ya kubuma siyajui,” alisema
Diamond.
Tujikumbushe kidogo
Mwaka jana, Agosti 6, Tiffah alizaliwa
na siku chache baadaye akalamba mkataba mnono wa Ubalozi wa Benki ya NMB
na maduka makubwa ya vitu vya watoto.
Post a Comment