PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: Mgogoro Kanisa Anglikana Wachukua Sura Mpya,Askofu Mokiwa Atishia Kupasua Jipu..!!!
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
Askofu wa Kanisa Anglikana Dayosisi ya Dar es Salaam, Dk Valentino Mokiwa amesema ataweka hadharani vitu anavyodai vitaonye...



Askofu wa Kanisa Anglikana Dayosisi ya Dar es Salaam, Dk Valentino Mokiwa amesema ataweka hadharani vitu anavyodai vitaonyesha ukweli wa mgogoro uliopo katika dayosisi hiyo anayoiongoza.

Amesema baada ya siku saba, atawasilisha kwa waumini vitu vitakavyoeleza ukweli wa mambo kuhusu mgogoro unaondelea sasa.

Hivi karibuni, Askofu Mkuu wa kanisa hilo, Dk Jacob Chimeledya alimtaka Mokiwa kujiuzulu kwa madai kwamba anatumia vibaya madaraka yake huku akimtuhumu pia kwa ubadhirifu wa fedha.

Hata hivyo, Askofu Mokiwa alikana madai hayo na kusema mgogoro huo unatengenezwa na adui zake jambo linawavunja mioyo waumini.

Jana, akiweka jiwe la msingi la Kanisa la Kigango cha Mtakatifu Simon na Yuda, lililopo Kimara Mavurunza ‘A’, Askofu Mokiwa alisema:

“Nipeni wiki  hii inayoaanza kesho (leo), nikichelewa wiki moja na nusu nitawaeleza ukweli; hakuna kitu kilichoibwa wala kukosewa, isipokuwa waliokosea wanataka kutuvuruga.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top