Njia bora Zaidi ya kuweza kuukimbia umaskini ni kufanya kazi
kwa bidii bila kuchoka mpaka pale ambapo utakapoona sasa unaelekea kufanikiwa
kiuchumi na kuwa na uhuru wa kipato chako halali
Watu wote waliofanikiwa kiuchumi wana siri moja tu nayo ni
nidhamu ya kujituma kila siku juu ya jambo ambalo wanadhani lina manufaa kwao
na maisha yao, wanajali sana muda wa kutenda kazi in above average attitude
ndio maana wengi wao huwai sana kuamka na kuchelewa kulala na muda wote huo
yupo bize kufanya kazi zake zinazompatia kipato chake halali muda wake wa
kupumzika ni mchache sana kama ana kampuni au mradi wake mara nyingi huwa wa
kwanza kufika kazini na pia huwa wa mwisho kuondoka huwa hawafikirii overtime
au siku ya mapumziko bali huifikiria kazi yake each and every day.
Hivyo kama ni mkulima jiwekee utaratibu wa kuwahi kufika
shambani kwako mapema sana asubuhi ufanye kazi zako, kama ni biashara uamke
mapema ufungue biashara yako na sio unafungua saa nne asubuhi hapo muda unakuwa
umekwenda sana na umepoteza wateja wengi mno kama umeajiriwa mahali fanya kazi
kwa uaminifu mkubwa na uwe na faida kwa huyo mwajiri wako tenda Zaidi ya
ulichopangiwa hii itakujengea utamaduni wa kuweza kujisimamia mwenyewe siku
ukifungua mradi wako lakini pia huna budi kuanzisha mradi wako mdogo utakaoweza kuusimamia mara baada ya kazi za mwajiri wako na kuweza kukuingizia
kipato chako cha pili kitakachokuongezea pato lako la siku
Miradi midogo midogo inayoweza kukuingizia kipato chako
mbali ya mshahara wa mwajiri wako ni kama ufugaji wa kuku au samaki, kilimo cha
mbogamboga na mingineyo unaweza kuiona ni midogo lakini ina nafasi kubwa sana
ya kukuongezea kipato chako cha siku na kukupa nidhamu kubwa ya matumizi ya pesa zako.
Kuna msemo usemao kuwa nyumba ya wavivu haiishiwi njaa huu
msemo wa wazee wa kale una maana kubwa ukitafakari kwa jicho la tatu walikuwa
wanamanisha kuwa wavivu yaani wao kila siku ni njaa na matatizo yasiyo na ukomo
ni kwa sababu moja tu kutokubali kujituma ipasavyo katika jambo linalowapa
kipato halali, kupenda starehe zisizokuwa na maana kupenda kulala na kuchelewa
kuamka na kutumia kipato chote akipatacho bila kukumbuka kesho atatumia nini na hawajui kabisa kanuni ya kujiwekea akiba.
Maskini wote duniani wana tabia zinazofanana kwanza
hawapendi kujifunza, huona kila kitu anakijua wana majivuno na dharau kwa watu
waliowazidi kiuchumi na kifikra na kusingizia vitu visivyokuwa na ushahidi kwa
watu waliofanikiwa mfano utasikia huyo bwana kafanikiwa kwa sababu ni freemason
au ni fisadi au ni mwizi au kamtoa mwanaye kafara, ukimuuliza una uhakika
utasikia hapana nilisikia kwa jamaa yake wa karibu au watu wote mtaani wana
sema hivyo hizi ni fikrabmbaya sana hazikupi uelewa wa kufanya kazi kwa bidii na kujikuta unaamini shortcut life which is very wrong cut.
Hata vitabu vya Mungu vinasisitiza kuwa asiyefanya kazi na
asile lengo la mstari huo ni kumfanya mwanadamu afanye kazi kwa bidii ili aweze
kupata mahitaji yake muhimu pasi na kumtegemea mwenzake yaani kila mmoja
akifanya kazi kwa bidii tutakuwa na maisha yenye furaha kwani utakuwa unauwezo
wa kujitegemea kwa asilimia kubwa na utaweza kutatua matatizo yako mwenyewe
Lazima tujifunze kutoka kwa waliofanikiwa kwa sababu njia
zao halali walizozitumia kufanikiwa kama nasi tutazitumia tutafanikwa mno na moja ya kanuni wanayotumia waliofanikiwa ni
mgawanyo wa matumizi ya kipato chao kama ifuatavyo
Kumbuka matumizi haya hupangwa kabla ya kuanza kutumia
kipato chako ulichokipata kwa kufanya kazi na au faida ya biashara yako
Jenga utamaduni wa kuweka kipato chako
chochote katika mpangilio huo hapo juu utafanikiwa na kuwa na nidhamu ya matumiziya
kipato chako na mwisho wa siku utafanikiwa kuukimbia umaskini.
Asante kwa kushiriki nami katika makala haya naamini kuna jambo moja la kukusaidia maishani mwako
NGOBOLE, Andrea Ashery
0755780131
ngoboleaa@gmail.com
facebook page princemediatz
instargram princemediatz
Post a Comment