PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: FANYA KAZI KWA BIDII ILI UUKIMBIE UMASKINI
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
NA: ANDREA NGOBOLE PMT Njia bora Zaidi ya kuweza kuukimbia umaskini ni kufanya kazi kwa bidii bila kuchoka mpaka pale ambapo uta...



https://scontent.fjnb2-1.fna.fbcdn.net/v/t1.0-9/15941125_1270380289720137_5143866078369843999_n.jpg?_nc_eui2=v1%3AAeG1jAEuzLY7-7LfRdvl7CW4CBOQPGf6yL5N3HGMif8FfE-1trtuAYotJ3C3VGwf_FgULsAuRY2O8DFMb7rO2Jx4VGqt86veKtiwEuz0tKc5rrUOfz2EiseGPZeQYe3gqBI&oh=2fb256ff23f46e0facf4dc22f2d63f7d&oe=58D5C5A8

Njia bora Zaidi ya kuweza kuukimbia umaskini ni kufanya kazi kwa bidii bila kuchoka mpaka pale ambapo utakapoona sasa unaelekea kufanikiwa kiuchumi na kuwa na uhuru wa kipato chako halali

Watu wote waliofanikiwa kiuchumi wana siri moja tu nayo ni nidhamu ya kujituma kila siku juu ya jambo ambalo wanadhani lina manufaa kwao na maisha yao, wanajali sana muda wa kutenda kazi in above average attitude ndio maana wengi wao huwai sana kuamka na kuchelewa kulala na muda wote huo yupo bize kufanya kazi zake zinazompatia kipato chake halali muda wake wa kupumzika ni mchache sana kama ana kampuni au mradi wake mara nyingi huwa wa kwanza kufika kazini na pia huwa wa mwisho kuondoka huwa hawafikirii overtime au siku ya mapumziko bali huifikiria kazi yake each and every day.

Hivyo kama ni mkulima jiwekee utaratibu wa kuwahi kufika shambani kwako mapema sana asubuhi ufanye kazi zako, kama ni biashara uamke mapema ufungue biashara yako na sio unafungua saa nne asubuhi hapo muda unakuwa umekwenda sana na umepoteza wateja wengi mno kama umeajiriwa mahali fanya kazi kwa uaminifu mkubwa na uwe na faida kwa huyo mwajiri wako tenda Zaidi ya ulichopangiwa hii itakujengea utamaduni wa kuweza kujisimamia mwenyewe siku ukifungua mradi wako lakini pia huna budi kuanzisha mradi wako mdogo utakaoweza kuusimamia mara baada ya kazi za mwajiri wako na kuweza kukuingizia kipato chako cha pili kitakachokuongezea pato lako la siku

Miradi midogo midogo inayoweza kukuingizia kipato chako mbali ya mshahara wa mwajiri wako ni kama ufugaji wa kuku au samaki, kilimo cha mbogamboga na mingineyo unaweza kuiona ni midogo lakini ina nafasi kubwa sana ya kukuongezea kipato chako cha siku na kukupa nidhamu kubwa ya matumizi ya pesa zako.

Kuna msemo usemao kuwa nyumba ya wavivu haiishiwi njaa huu msemo wa wazee wa kale una maana kubwa ukitafakari kwa jicho la tatu walikuwa wanamanisha kuwa wavivu yaani wao kila siku ni njaa na matatizo yasiyo na ukomo ni kwa sababu moja tu kutokubali kujituma ipasavyo katika jambo linalowapa kipato halali, kupenda starehe zisizokuwa na maana kupenda kulala na kuchelewa kuamka na kutumia kipato chote akipatacho bila kukumbuka kesho atatumia nini na hawajui kabisa kanuni ya kujiwekea akiba.

Maskini wote duniani wana tabia zinazofanana kwanza hawapendi kujifunza, huona kila kitu anakijua wana majivuno na dharau kwa watu waliowazidi kiuchumi na kifikra na kusingizia vitu visivyokuwa na ushahidi kwa watu waliofanikiwa mfano utasikia huyo bwana kafanikiwa kwa sababu ni freemason au ni fisadi au ni mwizi au kamtoa mwanaye kafara, ukimuuliza una uhakika utasikia hapana nilisikia kwa jamaa yake wa karibu au watu wote mtaani wana sema hivyo hizi ni fikrabmbaya sana hazikupi uelewa wa kufanya kazi kwa bidii na kujikuta unaamini shortcut life which is very wrong cut.

Hata vitabu vya Mungu vinasisitiza kuwa asiyefanya kazi na asile lengo la mstari huo ni kumfanya mwanadamu afanye kazi kwa bidii ili aweze kupata mahitaji yake muhimu pasi na kumtegemea mwenzake yaani kila mmoja akifanya kazi kwa bidii tutakuwa na maisha yenye furaha kwani utakuwa unauwezo wa kujitegemea kwa asilimia kubwa na utaweza kutatua matatizo yako mwenyewe

Lazima tujifunze kutoka kwa waliofanikiwa kwa sababu njia zao halali walizozitumia kufanikiwa kama nasi tutazitumia tutafanikwa mno  na moja ya kanuni wanayotumia waliofanikiwa ni mgawanyo wa matumizi ya kipato chao kama ifuatavyo


Kumbuka matumizi haya hupangwa kabla ya kuanza kutumia kipato chako ulichokipata kwa kufanya kazi na au  faida ya biashara yako

  Jenga utamaduni wa kuweka kipato chako chochote katika mpangilio huo hapo juu utafanikiwa na kuwa na nidhamu ya matumiziya kipato chako na mwisho wa siku utafanikiwa kuukimbia umaskini.
Asante kwa kushiriki nami katika makala haya naamini kuna jambo moja la kukusaidia maishani mwako


NGOBOLE, Andrea Ashery
0755780131 
ngoboleaa@gmail.com
facebook page princemediatz
instargram  princemediatz
  

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top