Msanii wa bongo fleva Darasa
ameweka wazi ule mstari wake wa "sio simba, sio chui, sio mamba" kwa
kusema Diamond hakupaswa kujiita simba kwani simba ni mnyama ambaye
anaweza kuuliwa anapozidiwa nguvu.
Darassa
"Ningekuwa Diamond nisingejiita simba, ninavyomuona Diamond ni zaidi ya Simba, kuna watu wanaua simba, simba, kajichanganya, kaingia kijijini kapotea, Diamond kwa kitu anachofanya ni zaidi ya simba, angeweza kujiita jina lingine lolote kubwa, kafanya vitu vingi sana". Amesema Darassa
Diamond
Darassa amemalizia kwa kusema wanyama wote ambao amewataja katika
wimbo wake hawaogopi kwa kuwa ana kitu kikubwa ndani yake na yeye ni
mwanaume na anajiamini kwa muziki wake anaofanya."Kwa upande wangu nimesema siyo simba, siyo chui siyo mamba, mamba ni mnyama anayetisha sana kwenye maji, simba anatisha sana porini, chui ni hunter mzuri, so katika vitu vyote ambavyo viko humo, mimi humo kote simo, ninacho kitu ambacho kinaweza kunifanya nikwambie aaaaah". Amemalizia Darassa
Post a Comment